Habari za Punde

Wizara ya Afya Zanzibar Yaandaa Semina ya Mapitio ya Mradi wa Maradhi Yasiopewa Kipaumbele Iliofanyika Katika Ukumbi wa Hoteli ya Visital Inn Jambiani.A

Washiriki mbali mbali wa Semina wakifanya mapitio ya Mradi wa kutokomeza Maradhi yasiopewa kipaumbele (Kichocho,Matende na Vikope) katika ukumbi wa Hoteli ya VISITAL INN iliopo Jambiani Mkoa wa kusini Unguija.
Washiriki mbali mbali wa Semina wakifanya mapitio ya Mradi wa kutokomeza Maradhi yasiopewa kipaumbele (Kichocho,Matende na Vikope) katika ukumbi wa hoteli ya visitak inn iliopo Jambiani Mkoa wa kusini Unguija. 
Baadhi ya Washiriki mbali mbali wa Semina wakiwa katika makundi wakipitia mapitio ya Mradi huo wa kutokomeza Maradhi yasiopewa kipaumbele (Kichocho,Matende na Vikope) katika ukumbi wa Hoteli ya VISITAL INN iliopo Jambiani Mkoa wa kusini Unguija.
Mwenyekiti wa Mpango wa kutokomeza Maradhi hayo kutoka  Shirika la Global Schistosomiasis Alliance (GSA) Dr Lorenzo Savioli,akizungumza na waandishi wa habari namna ya walivyodhamiria kuyatokomeza maradhi haya katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar.yanayokabiliwa na maradhi hayo. 
Mkurugenzi Maendeleo Mamlaka ya Maji Zanzibar Ndg. Mohammed Eliasa Mohammed akizungumza na Waandishi wa Habari,  namna walivyokusudia kuwapelekea Wananchi huduma ya Maji Safi na salama maeneo yote ambayo yamegundulika na maradhi ya kichocho hayana maji salama watafikisha huduma ya Maji safi na salama haraka iwezekanavyo .
Picha na Abdallah Omar Maelezo Zanzibar.


Na Ali Issa Maelezo Zanzibar.
Wizara ya Afya Zanzibar kupitia kitengo cha maradhi ya yasio pewa kipaumbele (kichocho,matende, na Vikope) kimo katika harakati za kuyatokomeza kabisa maradhi hayo katika maeneo ya Zanzibar.

Hayo yamesemwa leo huko Mkoa wa Kusini Unguja katika Hoteli ya visital inn Jambian na Dr.Khalifan Abdalla Mohamed wakati wa semina ya mapitio wa mradi huo uliomaliza muda wake wa kutokomeza maradhi hayo .

Amesema maradhi ya kichocho na matende yaliathiri sana wananchi wa visiwa vya zanzbar katika miaka ya thamanini na kupelekea wengine kupata maradhi ya matende hadi hii leo jambo ambalo kwasasa maradhi hayo yanaonekana kutoweka kutokana na jitihada za Serikali na washirika wake wa maendeleo kulivalia njuga tatizo hilo.

Amesema kwa sasa hali hiyo inaridhisha kwa kiasi kikubwa na sehemu zilizobakia ni chache kulitokomeza tatizo hilo

“Tuna tarajia kuyamaliza maradhi ya kichocho na matende kwani imekuwa nadra kupokea wagonjwa wa maradhi haya ispokuwa ni wale wale wagonjwa wa zamani tu walioathirika na matende,kichocho,na yapo baadhi ya maeneo ambayo hayajamalizika maradhi hayo katika maeneo ya gamba,kinyasini,moga,kizimkazi na kwa Pemba ni maeneo ya micheweni ”alisema DR Khalifan.

Nae Mwenyekiti wa mradi huo wa kutokomeza maradhi hayo kutoka Nchini geneva katika Shirika la Global Schistosomiasis Alliance Dr Lorenzo Savioli amesema mapitio ya semina hiyo ni kuangalia vipi kuisaidia Zanzibar kwa kuwapatia madawa na kufikia lengo la kuyatokomeza kabisa maradhi hayo.

Amesema wananchi wazitumie dawa hizo kwa rika zote na hazina matatizo yoyote bali zinapoza zaidi maradhi mengine kama vile mapele mabaka na mipasuko mwilini.

Alisema wazitumie dawa hizo na nifrusa kwao ,kwani nchini kwao dawa hizo ni ghali mno .
Nae mkurugenzi wa Maendeleo ya maji Zanzibar Mohammed Eliasa Mohammed alisema katika kuondoa tatizo la kichocho Zanzibar ni kuhakikisha kupeleka maji safi na salama katika maeneo yote ya zanzbar ili wananchi waweze kutumia maji safi na kuacha kutumia maji ya mito na mashimo.

Aidha alisema wanalazimika maji kuyatia dawa yakuulia vimelea vya maradhi hayo ili visiwe na nafasi ya kuathiri wananchi wanapo yatumia.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.