Habari za Punde

ZIRPP MONTHLY LECTURE

Dear Members and Friends,
 
I have the pleasure to kindly inform you that there will be another ZIRPP Monthly Lecture.
 
Chairperson: Mr. Muhammad Yussuf

Speaker: Mr. Enzi Talib Aboud
Subject: 53 Anniversary of the Zanzibar Revolution: Advantages and Disadvantages"
Date & Time: Saturday 28 January 2017; at 4:00 pm.
Venue: ZIRPP Office,Third Floor, behind Majestic Cinema (above ZANLINK
 
ABSTRACT: Mapinduzi ya Zanzibar ya tarehe 12 Januari 1964, yalifanyika mwezi mmoja tu baada ya Zanzibar kupata uhuru wake mnamo tarehe 10 Desemba 1963 kutoka kwa Mkoloni wa Kiingereza, na hivyo kuwashangaza wananchi wengi wa Zanzibar na hasa katika nchi za jirani, kama vile Tanganyika, Kenya, Uganda na duniani kote kwa jumla. Mambo mengi mazuri yametekelezwa baada ya mapinduzi chini ya Uongozi wa Mzee Abeid Amani Karume, Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar aliyetawala Zanzibar kuanzia mwezi Januari 1964 hadi Aprili 1972 alipouawa. Haya ni pamoja na kutoa huduma za afya na matibabu, elimu na makaazi bure kwa wananchi bila ya ubaguzi wowote ule.
 
Lakini, vile vile kuna mambo mengi ambayo hayakuwa mazuri yaliyofanyika chini ya Uongozi wa Mzee Karume na viongozi wengine waliofuata baada yake. Kuna wale wanaosema kuwa mapinduzi ya Zanzibar yamechangia sana katika kuleta Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar na hivyo kuiondolea Zanzibar uhuru wake wa kitaifa wa kujiamulia mambo yake yenyewe kitaifa na kimataifa.
 
Mwandishi wa habari mkongwe wa Zanzibar, Bwana Enzi Talib Aboud, atajaribu kuelezea kwa undani kabisa historia, faida na hasara zilizopatikana kutokana na Mapinduzi na jinsi ambavyo Zanzibar itakavyoweza kujiimarisha kisiasa, kiuchumi, kijamii na kimaendeleo na kujihakikishia kuwa mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 yanaendelezwa kwa faida na maslahi mapana ya Wazanzibari na Zanzibar kwa jumla na sio kwa faida na maslahi ya wachache. 
 
Tea, Coffee and Snacks will be served freely.
 
Please forward this message to anybody who may be interested. Those who would like to attend should send their email addresses and telephone numbers to: zirpp@googlegroups.com.
 
Please confirm your participation. You may bring one or two friends with you.
 
All are welcome.
 
 
Muhammad Yussuf
Executive Director
Zanzibar Institute for Research and Public Policy
P.O. Box 4523, Zanzibar, Tanzania;
Tel: +255 242 223-8474;
Fax: +255 242 223-8475;
Cellular: 0777 707820;
Website: www.zirpp.info

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.