Habari za Punde

Ligi daraja la Pili Wilaya ya Mjini Kati ya Timu ya Muembeladu na Gulioni Timu ya Muembeladu Imeshinda kwa Bao 3-2 Mchezo Uliofanyika Usiku Huu Uwanja wa Amaan Zanzibar

Wachezaji wa Timu ya Muembeladu wakishangilia bao lao la kwanza katika mchezo wa Ligi Daraja la Pili Wilaya ya Mjini Unguja mchezo uliofanyika usiku huu katika uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Muembeladu imeshinda mchezo huo dhidi ya Timu ya Gulioni kwa mabao 3-2.
Mshambuliaji wa Timu ya Muembeladu mwenye mpira Yahya Adinani akimpita beki wa Timu ya Gulioni Mussa Haji wakati wa mchezo wao wa Ligi Daraja la Pili Wilaya ya Mjini Unguja uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar usiku huu Timu ya Muembeladu imeshinda 3-2.
Beki wa Timu ya Muembeladu akiwa na mpira wakati wa mchezo wao wa ligi ya daraja la pili wilaya ya mjini mchezo uliofanyika uwanja wa amaan.
Mshambuliaji wa Timu ya Muembeladu Ali Seif akimpita beki wa Timu ya Gulioni Saadat Bakari.
Mshambuliaji wa Timu ya Muembeladu Ramadhani Haji akijaribu kumpita Beki wa Timu ya Gulioni Fahim Abdallah wakati wa mchezo wao wa Ligi Daraja la Pili Wilaya ya Mjini mchezo uliofanyika uiwanja wa amaan Zanzibar Timu ya Muembeladui imeshinda bao 3-2.
Mshambuliaji wa Timu ya Muembeladu Ramadhani Haji mwenye mpira akijaribu kumpiga chenga beki wa Timu ya Gulioni Fahim Abdallah wakati wa mchezo wao wa Ligi Daraja la Pili Wilaya ya Mjini Unguja mchezo uliofanyika uwanja wa amaan.  
Wapenzi wa Timu ya Gulioni wakiwa na simazi baada ya timu yao kufungwa katika mchezo wao wa Ligi Daraja la Pili Wilaya ya Mjini Unguja.
Mchezaji w Timu ya Gulioni Saadat Bakari akikokota mpira huku mchezaji wa Timu ya Muembeladu Mussa Haji akimfuta kujaribu kumzuiya wakati wa mchezo wao wa Ligi Daraja la Pili Wilaya ya Mjini Unguja uliofanyika usiku huu uwanja wa amaan Zanzibar. 
Wachezaji wa Timu ya Gulioni wakishangilia bao lao wakati wa mchezo huo. 
Wapenzi wa Timu ya Gulioni wakishangilia timu yao baada ya kusawazisha bao la kwanza katika kipindi cha kwanza katika dakika ya 44 ya mchezo huo uliofanyika uwanja wa amaan usiku huu.  
Wapenzi wa Timu ya Gulioni wakishangilia timu yao baada ya kusawazisha bao la kwanza katika kipindi cha kwanza katika dakika ya 44 ya mchezo huo uliofanyika uwanja wa amaan usiku huu. 
Benchi la ufundi la Timu ya Muembeladu wakifuatilia mchezo huo wa Ligi Daraja la Pili Wilaya ya Mjini.




 Watoto mashabiki wa Timu ya Muembeladu wakifuatilia mchezo huo.
Watoto wapenzi wa Timu ya Guliogi wakifuatilia mchezo huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.