Bi Shemsa Hakim akisimama mbele ya gari yake ta Teksi
NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.
Mwandishi Abdi Suleiman |
“KWA sasa huna vya kuniambaia juu kazi yangu hii!!!!!!!!!
kwangu ni kama kazi nyengine, nimekuwa nikipokea simu za wageni wanaohitaji
huduma yangu wakiwa Dar au Unguja ndio kwanza wanapanda ndege” aliniambia
Shemsa huku akitabasamu.
Mcheshi
na mchangamfu kwa kila mtu wakati wote utakapomuona, ni dereva anayetulia
wakati anapokuwa amepakiwa wateja na kuwapeleka sehemu wanazohitaji kwenda.
Shemsa
Hakim Khamis (40), si mrefu wala mfupi ni mtu wa wastani, mwenye uso mpana
wenye kungaraa kutokana na weupe wake, mchangamfu muda wote ikimtazama mara
anacheka na kuinamia chini.
Mwishoni
mwa mwaka 2016 alianza kazi ya udereva Taxi katika kituo cha Uwanja wa Ndege wa
Karume Pemba, bila ya kujali yeye ni jinsia gani na kazi hiyo ikiwa imezoeleka
kufanywa na wanaume.
“Kazi
hii ni kazi kama kazi nyengine ikishakuwa umejiamini kuifanya na bila ya kujali
maneno maneno ya watu, basi utafanikiwa chamsingi ni heshima inahitajika katika
kazi hiii” alieleza Shemsa.
Bila
ya kushawishiwa aliamua kujiingiza katika kazi hii ya Udereva wa Taxi katika
uwanjani wa Ndege, kwa lengo la kujiajiri mwenyewe na kuacha utegemezi wa mume
nyumbani.
Kwa
sasa Shemsa ameanza kujizoelea wateja kutoka sehemu mbali mbali zaidi wanawake
wenzake wanaofika Kisiwani Pemba, kulazimika kuhitaji huduma ya usafiri kutoka
kwake.
Mzaliwa
wa Chanjamjawiri mwaka 1977, alimaliza darasa la 10 mwaka 1989 katika skuli ya
Chanjamjawiri, baada ya wazee wake kutengana alishindwa kupata nafasi ya
kuendelea na masomo.
Anasema
alilazimika kukaa nyumbani kumuhudumia mama yake, ambae kwa wakati huo tayari
umri ulishamchukuwa, hali iliyofanya ndoto zake za kuwa rubani wa ndege kuanza
kupotea na kuingia katika biashara ndogo ndogo.
“Nililazimika
kupika Uji, Maandazi, vileja na biadhaa nyengine ndogo ndogo ili tuweze kupata
pesa za matumizi, muda ukafika nikapata mume akaniona” alisema.
Mwaka
1995 niliolewa ambapo hadi sasa sikubahatika kupata mtoto, tunapendana sana
mimi na mume wangu, yeye ni mfanya biashara na mimi ni dereva Tax tunasaidiana
maisha.
Udereva
Tax ulikuja baada kuwa na usafiri wangu binafsi, mwanzo nilimpa mtu kuendesha
lakini maslahi yalikuwa magumu kupatikana nimeamua kuendesha mwenyewe na sasa nimejuwa
faida zake, Changamoto zake.
Pia
alimpa mtu kumuendeshea na kutokuona maslahi yoyote, kulazimika kuuchukuwa
mwenyewe na kujuwa kama kuna faida au laaa, aliweza kushirikiana na mumewe na
kuelewana.
“Mafunzo
haya ya udereva nimeyapata kutoka kwa shemegi yangu hapa chake chake, alikuwa jioni
jioni akinifundisha gari, nimefuata taratibu zote katika upataji wa leseni na
sasa naweza kuendesha gari na kupeleka abiria sehemu yoyote ile” alisema.
Tokea
kuingia katika kazi hii sijapata na matatizo yoyote, madereva wenzakengu
wamekuwa wakinisaidia kwa kiasi kikubwa, kunipa mbinu za kupata wateja licha ya
kuwa kuna zamu zake hapa, lakini ikifika zamu yangu wanazungumza na abiria na
kuniambia nimpeleke sehemu fulani na nauli yake kiasi fulani basi.
Tokea kuwepo hapa lakini bado sijawahi kupata abiria mzungu au mgeni anayehitaji
kwenda makangale, zaidi ni wa hapahapa mjini akitokea nitampeleka.
“Tayari
wanawake wenzangu wameweza kufurahia na wako tayari kuungana na mimi katika
kazi ya udereva wa Tax, hapa chamsingi heshima na nidhamu ndio kitu muhimu
katika kazi hizii, usafi wa gari na dereva mwenyewe” alisema.
Kuhusu
masuala ya Familia Shemsa anasema, Mumewe akiwepo hulazimika kwenda kazini
mchana asubuhi huwepo nyumbani, kwa ajili ya kushughulikia mambo ya familia,
akiwa hayupo hulazimika kwenda kazini asubuhi ili kuwahi namba kama walivyo
wengine” alisema.
Mitazamo
iliyopo mimi naichukulia kama hali ya kawaida tu, kazi ni kazi tu pesa ikiwa
inapatikana, kuhusu abiria wasiokuwa na nidhamu, anasema ni heshima ya mtu,
ambapo kwa sasa anajifundisha lugha ya Kiengereza kidogo kidogo.
Changamoto
anazokumbana nazo, baadhi ya abiria wanapowakodisha gari kwa siku nzima,
wengine kutokuwalipa pesa zao wapo wanaowalipa na wengine sio waaminifu na
kazi.
Shemsa
anasema biashara inavipindi, vipo vipindi biashara inakuwa nzuri na vipo
vipindi biashara inakuwa mbaya, hata pesa ya mafuta ulioweka kwa siku ile
huipati lakini ndio biashara.
Akifafanua
malengo yake anasema ni kununua gari nyengine na kuwa na gari mbili, huku
akiwataka wanawake wenzake kujitokeza kumuunga mkono katika fani hiyo.
Mdhamini
wa kamisheni ya Utalii Pemba, Suleiman Amour Suleiman, anasema sekta ya Utalii
Pemba inazidi kuimarika baada ya kujitokeza kwa dereva Tax Mwanamke.
Uwepo
wa Shemsa katika Tax imefikisha madereva Tax 44 wanaume 43 na Mwanamke mmoja,
ambapo sera ya Utalii kwa wote imeanza kutekelezwa kwa vitendo.
Anasema
Shemsa ataweza kuwa ni moja ya chanzo kikubwa cha kushajihisha wanawake kuona
kwamba kazi ya Tax ni sawa na kazi nyengine.
Mdhamini
anasema wakati umefika wa kuona mabadiliko katika sekta ya Utalii, hasa kwa
madereva Tax wanaochukuwa wageni katika sehemu mbali mbali za Kisiwa Cha Pemba
kuwepo akinamama.
“Kazi
ni kazi tu ikishekuwa ni yahalali basi hupaswi kuchagua kazi, Wengi sasa
wanamtizama Shemsa atamudu kazi hii, ili na wawo waweze kuingia na kuanza
kuchukuwa abiria” alisema.
Nifaraja
sasa kuona lile lengo la serikali la utalii kwa wote limeanza kutoa matunda,
kushiriki kwa wanawake dereva Tax kupeleka wageni, ikiwa utalii unatoa ajira
sasa imeanza ya kuendesha magari na kupeleka wageni, sekta ya utalii imepiga
hatua pemba.
Aidha
alimtaka Shemsa kutokuvunjika moyo na kunufaika na keki ya sekta ya utalii,
kujitahidi kuwa nadhifu ili kuweza kupata abiria kwa wingi na kuongeza pato
lake.
Mdhamini
wa Magari ya Kukodishwa Mkoa wa kusini Pemba, ambaye pia ni dereva wa Tax
Abdalla Ali Abdalla, alisema PESTA
wamefurahia sana kuona sasa Pemba inadereva TAX mwanamke katika Uwanja wa
Ndege.
Uwepo
wake wamepiga hatua na ndio dereva wa kwanza kwa Pemba Tax Mwanamke kujitokeza
kuchukuwa wageni, jambo ambalo ni lakujivunia.
Hata
hivyo aliwataka wanawake wengine kujitokeza, katika kumuunga mkono Shemsa
katika mkazi yake ya Udereva Tax, ili kuachana na dhana mbaya kwamba kazi za
udereva ni wanaume tu.
Mkuu
wa Mkoa wa kusini Pemba Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla, alisema anafarajika sana
kuona Zanzibar kuwepo kwa dereva wa kwanza Tax katika kisiwa Cha Pemba.
Kujitokeza
kwake ni kuonyesha mfano kwa wanawake wenzake, kutokubweteka na kuchagua kazi
za kufanya kwani kazi yoyote ni kazi kitu kizuri ni mtu kupata chumo la halali.
“Shemsa
amejitolea kuwa Dereva Tax hapa Pemba, ni mwanamke wa kwanza lakini wenzetu
bara utawaona wanawake mpaka makondakta wa mabasi ya mwendo kasi, wapo madereva
pia hili ni jambo la kujivunia Pemba” alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Hata
hivyo amewataka wanawake wenzake kujitokeza katika kazi na kuacha tabia ya
kuchagua kazi, kwani dunia sasa imebadilika kutokana na ukosefu wa ajira.
Mwanaharakati
wa Masuala ya Wanawake Pemba kutoka TAMWA, Jitihada Abdalla, alisema upo wa
Shemsa ni Jambo la kufurahia, wanawake wameanza kujitambua na kufanya kazi kama
walivyo wanaume.
Kitendo
cha kuchukuwa watalii ni kitendo kizuri, hii inaonesha wanawake wanaweza
wakiwezeshwa pale wanapopatiwa fursa, huku akiwataka wasibweteke na kuona ni
watu wakuolewa na kutunza familia, bali wanapaswa kushiriki shuhuli mbali mbali
za kijamii ili waweze kupata kipato na kuondokana na utegemezi.
TAMWA
imekuwa ikiwapa taaluma wanawake ya kushiriki katika mambo mbali mbali ikiwemo
kujitambua, nao wananchango mkubwa katika jamii.
Mwandishi
wa makala hii anapatikana kwa EMAIL:abdisuleiman33@gmail.com
0718968355.
No comments:
Post a Comment