Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo na Balozi mdogo wa China aliepo Zanzibar Xie Xiaowu wakisaini hati ya makabidhiano ya dawa zilizotolewa Serikali ya watu wa China.
Wafanyakazi wa Bohari Kuu ya Dawa Zanzibar na wanafunzi wa fani ya ufamasia wakifuatilia sherehe ya kukabidhiwa dawa zilizofanyika Bohari Kuu ya Maruhubi.
Mkurugenzi wa Bohari Kuu ya Dawa Zanzibar Zahran Ali Hamadi akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kuboreka kwa hali ya dawa Zanzibar baada ya Waziri wa Afya Zanzibar kukabidhiwa msaada wa dawa kutoka Serikali ya watu wa China.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo.
No comments:
Post a Comment