Habari za Punde

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Masauni Atembelea Bandari ya Zanzibar, Aagiza Jeshi la Polisi Kushirikiana na Uongozi wa Banndari Kudhibiti Uingiaji wa Dawa za Kulevya Zanzibar.

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,akitembea kuelekea sehemu inayokaguliwa mizigo wakati wa ziara ya kutembelea Bandari ya Zanzibar,ikiwa na lengo la kukagua mifumo ya udhibiti wa uingizwaji wa Dawa za Kulevya, huku akiliagiza Jeshi la Polisi Zanzibar, kushirikiana na Uongozi wa Bandari kuhakikisha ukaguzi wa mizigo unafanyika ili kukomesha uingiaji wa dawa hizo ambazo humaliza nguvu kazi ya Taifa.Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe.Mohamed Ahmada Salum na anayefuatia ni Mkurugenzi Mkuu Shirika la Bandari Zanzibar, Kapteni Mstaafu Abdula Juma
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa ziara yake kutembelea Bandari ya Zanzibar, ikiwa na lengo la kukagua mifumo ya udhibiti wa uingizwaji wa Dawa za Kulevya akiliagiza Jeshi la Polisi Zanzibar kushirikiana na Uongozi wa Shirika la Bandari Zanzibar, kuhakikisha ukaguzi wa mizigo unafanyika ili kukomesha uingiaji wa dawa hizo ambazo humaliza nguvu kazi ya Taifa.Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mhe.Mohamed Ahmada Salum na anayefuatia ni Mkurugenzi Mkuu Shirika la Bandari Zanzibar, Kapteni Mstaafu Abdula Juma
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akikagua jinsi ya ukaguzi wa mizigo unavyofanyi kakupitia komputa wakati wa ziara yake kutembelea Bandari ya Zanzibar. kukagua mifumo ya udhibiti wa uingizwaji wa Dawa za Kulevya,na kuliagiza Jeshi la Polisi Zanzibar kushirikiana na Uongozi wa wa Shirika la Bandari kuhakikisha ukaguzi wa mizigo unafanyika ili kukomesha uingiaji wa dawa za kulevya kupitia bandarini na kutumika kwa vijana nguvu kazi la Taifa.Kulia ni Afisa wa Bandari anayeshughulikia ukaguzi, Adam Masoud.
Mfanyakazi wa kitengo cha mizigo Bandari ya Zanzibar, Saleh Masoud akikagua moja ya mzigo ya abiria wanaoingia kupitia bandari hiyo ambapo Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,ameliagiza Jeshi la Polisi Zanzibar kushirikiana na Uongozi wa Bandari hiyo kuhakikisha ukaguzi wa mizigo unafanyika ili kukomesha uingiaji wa Dawa za Kulevya ambazo zimekuwa zikiharibu nguvu kazi ya Taifa
Mkurugenzi Mkuu Shirika la Bandari Zanzibar, Kapteni Mstaafu Abdula Juma (wa pili kushoto), akimsikiliza Naibu Waziri Wizara wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati wa ziara yake kutembelea bandari ya Zanzibar. Kukagua mifumo ya udhibiti wa uingizwaji wa Dawa za Kulevya huku akiliagiza Jeshi la Polisi kushirikiana na Uongozi wa Bandari kuhakikisha ukaguzi wa mizigo unafanyika kwa makini  ili kukomesha uingiaji wa dawa hizo ambazo humaliza nguvu kazi ya Taifa.Wakwanza kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe.Mohamed Ahmada Salum na wakwanza kulia ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar,  Johari Masoud Sururu.
Kifaa cha kubebea kontena kikiwa kimebeba kontena tayari kupelekwa kwenye mashine maalumu ya ukaguzi ambayo hutumia mionzi kukagua mzigo uliopo ndani,ambapo Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameliagiza Jeshi la Polisi kushirikiana na Uongozi wa Bandari ya Zanzibar kukagua mizigo yote inayoingia ili kudhibiti uingiaji wa Dawa za Kulevya Visiwani Zanzibar. 
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.