Habari za Punde

Ndege Mpya ya Shirika la Ndege la Ethiopia Airline ya Airbus A350 Yawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar

Kuwepo kwa usafiri wa ndege ya Abiria ya Airbus A350 kutoka Shirika la Ethiopian Airlines, na kuunganisha safari  zake hadi Zanzibar, kutapanua wigo wa ujio wa watali nchini.
Ndege hiyo mpya yenye uwezo wa kuchukua abiria 345, iliyoundwa kwa teknolojia ya juu zaidi, ni ya  kwanza Barani Afrika, ambapo kwa mara ya kwanza  imewasili katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume, jana ikitokea mjini Addis Ababa, Ethiopia – Kilimanjaro – Zanzibar.
Lengo la safari hiyo, ni kuitangaza ndege hiyo, ikiaminika itakuwa na mchango mkubwa katika  uimarishaji wa sekta ya  utalii nchini.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.