STATE
HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Pemba 17.03.2017

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Ali Mohamed Shein amewataka vijana wa
CCM, Kiswani Pemba kuyatumia mashindano ya mpira wa miguu yalioanzishwa na
chama hicho kwa kuendeleza amani,mshikamano udugu, umoja, na mapenzi miongoni
mwao na sio kugombana.
Dk. Shein ambaye pia,
ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, aliyasema hayo leo huko katika ukumbi Skuli
Sekondari ya Fidel Castro, Mkoa wa Kusini Pemba mara baada ya kukabidhi vifaa
vya michezo ya vijana kwa ajili ya maandalizi ya Ligi ya Mpira wa Miguu kwa
Timu 18 za Kisiwani Pemba ikiwa na lengo la kusherehekea mwaka mmoja tokea kuapishwa
kwa Dk. Shein kuwa Rais wa Zanzibar awamu ya pili sambamba na kusherehekea
miaka 40 ya kuzaliwa kwa CCM.
Dk. Shein aliwataka
vijana wa CCM watakaoshindana katika ligi hiyo kutofanya mashindano hayo kuwa
sehemu ya mapambano na kuwataka kufuata sheria na taratibu za mpira wa miguu
huku akiwasisitiza kuwafuata sheria 17 za soka duniani ili wacheze vizuri.
Katika maelezo yake,
Dk. Shein aliwaeleza vijana hao pamoja na wanaCCM waliohudhuria katika hafla
hiyo kuwa michezo ni nidhamu na kuongeza kuwa chama cha CCM ndicho
kinachofundisha watu nidhamu, na kutoa pongezi za pekee kwa Mwakilishi wa Jimbo
la Uzini Mohamed Raza kwa kuyadhamini mashindano hayo.
Aidha, Dk. Shein
alitumia fursa hiyo kwa kujipongeza kwa niaba ya Wazanzibari na Watanzania wote
kwa jumla kwa Zanzibar kupata uwanachama wa CAF huku akitoa wito kwa viongozi
wa ZFA kutambua kuwa huu si wakati wa kulumbana na kupelekana mahakamani.
Alisema kuwa hiyo ni
ishara ya kuelekea FIFA hivyo, aliutaka uongozi wa ZFA kuachana na masuala ya
kupelekeana mahakani na iwapo watafanya hivyo Zanzibar inaweza kutolewa na kuwa
aibu kwa Zanzibar na Jamhuari ya Muungano wa Tanzania kwani juhudi kubwa
imepita hadi kufikia hapo.
Dk. Shein alisema kuwa
miaka mingi Zanzibar ilikuwa ikitafuta nafasi ya uwanachama wa CAF na hivi sasa
tayari imeshakuwa mwanachama halali, hivyo aliwataka viongozi wa ZFA watambue
kuwa huu si wakati wa malumbano badala yake ni wakati wa kuhakikisha Zanzibar
inarudi katika historia yake ya soka.
“Kufika hapa tulipofika jana ni jitihada za Zanzibar, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania viongozi mbali mbali wa Serikali na Mpira, sasa kazi iliyobakia kuweka pembeni mambo yasiyostahiki katika michezo”alisema.
“Wapi na wapi masuala ya mpira kwenda mahakamani, wakifanya masihara
hicho chama cha CAF hakitokubali kwa mambo hayo, itakuja kuwa ni aibu
kwa Zanzibar, Fifa hawakubali masuala hayo”alisema.
Aliwataka viongozi wa ZFA kuwa makini na kutambua kuwa wao ni viongozi
kwa ajili ya soka la Zanzibar na kuachana na mambo yao binafsi huku akisisitiza kuwa ZFA iongoze mpira na kuepukana na masuala ya kisiasa ndani ya chama hicho.
Pamoja na hayo, Dk. Shein aliwataka wanaCCM kuendelea na shughuli zao kama kawaida na wenye kazi kufanya kazi zao, wanaosoma waendelee kusoma na waliokuwa hawana kazi Serikali anayoiongoza imo katika juhudi za kuhakikisha wanapata ajira lakini kubwa ni kuepuka maneno ya kizushi kuwa kuna serikali itakuja kuiondoa madarakani serikali iliyopo ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Alisisitiza kuwa kauli hizo ni za kuzibeza na
kuwataka wanaCCM wasihadaike na
waendelee kukiimarisha chama chao na kueleza kuwa hakuna uchaguzi hadi mwaka
2020 na serikali iliyopo madarakani itaendelea kuongoza hadi uchaguzi huo
utakapofika.
Aidha, Dk. Shein aliwataka vijana na wananchi wote
kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi ili
kumuepusha na maradhi yasioambukizika na ndio maana ameiweka Januari mosi ya
kia mwaka kuwa ni siku ya mazoezi kitaifa.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Abdalla Juma
Abdalla Mabodi, alitumia fursa hiyo kutoa shukurani zake kwa uteuzi huo
alioupata hivi karibuni na kuelez furaha yake kwa Zanzibar kupata uwanachama wa
CAF kwani hatua hizo ni katika utekelezji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM katika
suala zima la michezo.
Alisema kuwa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzbar bado iko madarakani na inaendelea kuongoza nchi na
kuwataka wanaCCM nKatika hotuba yake Dk. Shein aliwataka vijana washindane
katika mchezo huo na wala wasigombane kwani lengo la michezo pamoja na kuanzishwa
kwa mashindano hayo ni kujenga umoja
baina yao.
Dk. Shein aliwataka
vijana hao wacheze vizuri ligi hiyo ili kuendelea kukipa heshima na mapenzi
chama chao cha CCM na kueleza kuwa Ilani ya chama hicho ina vifungu
vinavyoeleza kutekelezwa kwa sekta hiyo ya michezo.
Aliongeza kuwa
mashindano hayo yana lengo la kuimarisha chama, kutoa vipaji kwa vijana na
kuwataka viongozi wa Majimbo kuwaunga mkono na kuwasaidia vijana wao
watakaoshiriki katika ligi hiyo kwani na wao wanawajibu wa kufanya hivyo.
Mapema Mdhamini wa
mashindano hayo, Mohammed Raza alisisitiza azma yake ya kuazisha na kuyadhamini
mashindano ya mpira wa miguu kwa skuli zote za mikoa yote ya Zanzibar kwa
kushirikiana na Serikali pamoja na Wizara husika.
Raza pia, aliahidi kutoa
zawadi ya gari kwa mshindi wa kwanza katika mashindano hayo kisiwani Pemba
pamoja na kutoa vifaa kwa michezo mengine yote ambayo itashindaniwa mbali na
mpira wa miguu ikiwemo mpira wa pete, mpira wa kikapu, mpira wa meza na michezo
mengineyo.
Katika taarifa ya Ligi
hiyo iliyosomwa na Bakar Hemed Bakari
kuwa lengo la mashindano hayo ni kusherehekea miaka 40 ya kuzaliwa kwa
CCM, kuinua vipaji vya vijana katika mchezo wa mpira wa miguu sambamba na
kuunga mkono kauli ya Dk. Shein ya kutaka Zanzibar iwe na vuguvugu la michezo
kwani wanaamini kuwa hoja hiyo imelenga utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya
CCM.
Vijana hao pia,
walitoa salamu zao za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania John
Pombe Magufuli na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein kwa jitihada zao za
kupambana na biashara haramu ya madawa ya kulevya na kuahidi kuwa wakiwa wao ni
vijana watawaunga mkono viongozi hao katika mapambano hayo.
Mshindi wa kwanza wa
mashindano hayo atapata kikombe, gari na nishani ambapo mshindi wa pili atapata
milioni tatu na mshindi wa tatu atapata milioni mbili pamoja na zawadi nyengine
zitakazotolewa katika mashindano hayo.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address:
2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment