Habari za Punde

Spika wa BLW Mhe. Zuberi Maulid Amesema Mashirikiano ya Pamoja Yanahitajika Kupinga Vitendo vya Udhalilishaji.

Na Himidi Choko.BLW.
Zanzibar                                                                   Machi 16, 2017
Spika wa Baraza la Wawakilishi  Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid amesema  mashirikiano ya pamoja kwa makundi yote  yanahitajika ili kupinga vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia na watoto pamoja na matumiziya dawa za kulenya hapa nchini.
Akizungumza na wasanii wa Binti Filamu waliongozwa na Ngumbagme Misayo (Thea)  huko Afisini kwake Chukwani, Spika Maulid amesema  vitendo hivyo hivi sasa vinaonekana kushamiri katika jamii   hasa kwa watoto wadogo  na wafanyaji wamo katika jamii.
Hivyo Spika Maulid amesema  makundi ya kijamii kama vile  viongozi wa dini, wanasiasa na wasanii wanawajibu mkubwa  wa kuelimisha   juu ya madhara ya vitendo hivyo.
Amesema kwa kua  makundi hayo  yanaushawishi mkubwa katika jamii ni vyema yakaendelea kutoa elimu  juu ya ubaya wa vitendo hivyo hatimae vipungue na kutokomezwa kabisa.
Amesema miongoni mwa matokeo mabaya ya vitendo hivyo ni kuathika kwa nguvu kazi  kisaikolojia  na maambukizi ya magonywa ya zinaa  hivyo suala la udhalilishaji wa kijinsia  na watoto pamoja na matumizi ya dawa za kulenya linafaa kupigwa vita kwa nguvu zote.
Nao wasanii wa Binti Filamu  wamesema wataendelea kuelimisha jamii juu ya madhara ya vitendo hivyo kwa kutumia majukwaa yao  ili kulinusuru taifa  na balaa la kuwa na viongozi wasiokua na maadili hapo baadae.

Mazungumzo hayo pia yamehudhuriwa na Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi ambae pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wawakilishi Wanawake zanzibar UWAWAZA mhe  Mgeni Hassan Juma.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.