Habari za Punde

Taarifa Kwa Wateja Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) inawatangazia Wateja Wake Kubadilisha Kadi za ATM.

THE PEOPLE’S BANK OF ZANZIBAR

Wapendwa  wateja  wetu,
Tunachukua fursa hii kuwataarifu kuwa Benki Kuu ya Tanzania imeagiza benki zote kutumia kadi za kisasa za ATM (EMV Chip Based Cards) zenye  teknolojia ya hali ya juu katika utunzanji  wa kumbukumbu za mteja ili kudhibiti uhalifu na wizi kupitia ATM.
Kutokana na agizo hilo uongozi wa  Benki  unawaomba wateja wetu  kurudisha ATM Kadi za zamani na kununua kadi mpya za kisasa (EMV Chip Based  Cards ) kupitia matawi ya Benki . Mwisho wa matumizi ya ATM kadi za zamani ni tarehe 30 Juni 2017.
Kwa maelezo zaidi juu ya ununuwaji wa kadi mpya (EMV Chip Based Cards ) tafadhali tembelea katika sehemu ya huduma ya wateja katika matawi yetu
Benki  tunaendelea  kukupa huduma  bora katika kila sekta .
Benki ya watu ,Chaguo la watu .

Mkurugenzi Mtendaji
PBZ BANK LTD
S.L.P 1173
Zanzibar
Tanzania 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.