Habari za Punde

Zoezi la Operesheni Viroba Laendelea Sehemu Mbalimbali Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Maafisa wa Serikali wakiwa nje ya moja ya duka lililokutwa na pombe kali ambayo Serikali imepiga marufu kutumika mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria toka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw. Manchare Heche akionesha kwa waandishi wa habari moja ya pombe kali aina ya kiroba original zilizokamatwa wakati wa operesheni inayoendelea mapema leo hii jijini Dar es Salaam wakati wa siku ya nne ya operesheni ya kusaka wasambazaji wa kinywaji hicho ambacho Serikali imepiga marufuku kutumika.
Mwanasheria toka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw. Manchare Heche akionesha kwa waandishi wa habari moja ya pombe kali aina ya kiroba original zilizokamatwa wakati wa operesheni inayoendelea mapema leo hii jijini Dar es Salaam wakati wa siku ya nne ya operesheni ya kusaka wasambazaji wa kinywaji hicho ambacho Serikali imepiga marufuku kutumika.
 Afisa Afya toka Manispaa ya Kinondoni Bw. John Kijumbe (kilia) akichukua maelezo toka kwa mmiliki wa duka la kuuza vinywaji la Vunja Bei salasala Store Bw. Oscar Mujuni (katikati) wakati wa opereshe ya kusaka wauzaji wa pombe kali aina ya viroba ambayo Serikali imepiga marufuku matumizi yake, kushoto ni Mwanasheria toka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw. Manchare Heche.
Mwanasheria toka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw. Manchare Heche akifunga moja ya duka la jumla la vinywaji mara baada ya msimamizi wa duka hilo kuwakimbia maafisa wa Serikali wakati wa opereshe ya kusaka wauzaji wa pombe kali aina ya viroba ambayo Serikali imepiga marufuku matumizi yake mapema hii leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku ya nne ya operesheni hiyo.
Mwanasheria toka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw. Manchare Heche akionesha kwa waandishi wa habari moja ya pombe kali aina ya Nguvu zilizokamatwa wakati wa operesheni inayoendelea mapema leo hii jijini Dar es Salaam wakati wa siku ya nne ya operesheni ya kusaka wasambazaji wa kinywaji hicho ambacho Serikali imepiga marufuku kutumika.
 Baadhi ya shehena ya pombe kali aina ya kiroba zilizokamatwa katika ghala la Kampuni ya Love Kira Enterprises lililopo Wazo jijini Dar es Salaam mapema hii 
 Msimamizi wa ghala la Love kira  Enterprises lililopo Wazo Bi. Sia Mboya (kushoto) akitoa maelekezo kwa Mwanasheria toka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw. Manchare Heche (katikati) wakati wa operesheni ya kuondoa pombe hiyo katika soko, kulia ni Afisa Afya toka Manispaa ya Kinondoni Bw. John Kijumbe.
 Gari lililokutwa limebeba pombe kali aina ya kiroba original likiwa limeegeshwa nje ya duka kuuza vinywaji la Love Kira lililopo Wazo jijini Dar es Salaam mapema hii leo.
Picha zote na Eliphace Marwa - Maelezo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.