Habari za Punde

shindano la Shika Ndinga linaloendeshwa na kituo cha redio cha Efm na kudhaminiwa na Kampuni ya Zantel

Mmoja kati ya majaji katika shindano la Shika Ndinga linaloendeshwa na kituo cha redio cha Efm na kudhaminiwa na Kampuni ya Zantel Said Mkumba (kulia) akimwonyesha kadi ya njano mmoja ya washiriki katika mwendelezo wa kampeni ya ‘Shika Ndinga’ iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Mwinjuma Mwananyamala jijini Dar es Salaam. Washiriki wawili kila mmoja alijinyakulia pikipiki yenye thamani ya Sh1.9 milioni baada ya kuibuka washindi.  Washiriki watano kwa upande wa wanawake na watano kwa upande wa wanaume walifuzu hatua ya mchujo. 
Washirikiwa shindano la Shika Ndinga linaloendeshwa na kituo cha redio Efm na kudhaminiwa na Kampuni ya Zantel wakichuana katika mwendelezo wa kampeni ya Shika Ndinga iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Mwinjuma Mwananyamala jijini Dar es Salaam. Washiriki wawili kila mmoja alijinyakulia pikipiki yenye thamani ya Tsh1.9 milioni baada ya kuibuka na ushindi.  Washiriki watano kwa upande wa wanawake na watano kwa upande wa wanaume walifuzu hatua ya mchujo. 




No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.