Habari za Punde

Nasiha za Bi Hekima: Chondechonde mafundi, mnatengeneza au mnaharibu?

Na Bi Hekima

Ijumaa nyingine yakupeana nasiha za ukweli. 

Tunapenda kukazania yasio na tija wakati masuala muhimu tunayafunika nyasi au chini ya jamvi.

Juzi juzi tu tumeadhimisha Mei Day. Wako wakulima waliokosoa hali ya kushereheka kinachowafaidisha wafanya kazi wa ajira rasmi tu tena sana sana walio serikalini.

Kwa upande wangu sijafurahishwa na mtindo wa kuhakiki hao wafanyakazi wanaotaka kutetewa na kuhudumiwa ni wepi? 

Sijui wenzangu mmeingia katika sehemu ipi ya huduma mkahisi mmehudumikiwa?

 Sijui lini mlililamika jambo mkahisi mmesikilizwa? 

Hao wa huduma za lazima washakoslewa sana. Maadui wangu mimi binafsi ni hii kada inayojiita ya mafundi tena wakujitegemea.

Naona karibuni neno hili litawekwa chini ya uangalizi wa usalama wa taifa na hakika wanastahili hilo. 

Hata hivyo nakiri kuwa kwa kiwango kikubwa labda hata asilimia 90% kada hii inaakisi waswahili na watanzania kwa ujumla wao.  Hawajali cha mtu unaweza kutoa kitu chako ulojinyima ili kipatikane kipate kutumika basi fundi akakiharibu na bado akataka alipwe wanawake wanalijua hili hasa na washoni ambao kutwa wanawaharibia vitambaa vyao.

Unaweza panga programu yako kuwa kazi ifanyike na imalize katika muda fulani wakaamua wao lini kuimaliza hata kama miaka 2 baadaye alimradi kiporo chake ndo mtaji wake wa pesa za dharura. Wengi wa mafundi bila kujali katumika miaka mingapi kukadiria hawaelewi na  huwa najiuliza kama kweli hawaelewi au ndo njama za kukula?

 Unawaleta kufanya kazi sehemu safi wakimaliza wakakupa kazi kumi za ziada ikiwemo ya usafi na matengenezo mengine ambayo wameyasababisha kwa kiwango chao uduni cha kazi. 

Na kila fundi mjuaji. Kazi anaijua na kuiweza yeye tu sio waliomtangulia! Hawataki kuelekezwa hata na wewe mwenye mali! Hawataki kukosolewa badala yake wanataka ujishushe katika matarajio yao ya mkono kwenda kinywa kwa tumbo si kukidhi matarajio yako.

Mafundi mahodari kuruka kazi mmoja kwenda nyengine bila ya kuwa na nia ya kuifanya kazi yenyewe. Wao lengo lao ni kula kilaini.

Ingawa mafundi wengi hujitia khamsa salawati na mwadhini hampiti bado sijaona fundi asiye mswahili na inaskitisha pale raia wanapoikubali hii hali kama kuwa ni kawaida au haiepukiki. 

Jamii nzima tunaendeshwa na watu (eti fundi yaani mtengenezaji) ambao wengi wao uwezo wao ni kama huo unaoonekana...👇Tupoe!  

                      

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.