Habari za Punde

Wafanyakazi wa ZANTEL Watembelea Kituo cha Polisi Oysterbay Katika Kuadhimisha Siku ya Afya na Usalama Mahala Pakazi Duniani.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin akizungumza na wafanyakazi wa Zantel mara baada ya wafanyakazi hao kuhitimisha matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani. Hafla ilifanyika katika makao makuu ya Kampuni hiyo Msasani jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma.
Askari wa Usalama barabarani, Wilaya ya Kinondoni S/SGT Rehema (kulia) akieleza kuhusu masuala ya usalama barabarani kwa wafanyakazi wa Zantel katika kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki mara baada ya wafanyakazi hao kukamilisha matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani. Waliokaa Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa kikosi cha Usalama barabarani wa Wilaya ya Kinondoni ACP Theopista Mallya na Afisa Mkuu wa masuala ya kiufundi Zantel, Larry Arthur.
Kamanda wa Polisi wa kikosi cha Usalama barabarani wa Wilaya ya Kinondoni, ACP Theopista Mallya akizungumza na wafanyakazi wa Zantel walipomtembelea katika kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki mara baada ya wafanyakazi hao kukamilisha matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani. Kulia ni Afisa Mkuu wa masuala ya kiufundi Zantel, Larry Arthur.

Mkuu wa Kitengo cha Intaneti na Simu wa Kampuni ya Mawasiliano Zantel, Hamza Zuheri (Kushoto) akifafanua jambo kwa Kamanda wa Polisi wa kikosi cha Usalama barabarani wa Wilaya ya Kinondoni, ACP Theopista Mallya (Wa pili kulia) ambapo wafanyakazi wa Kampuni hiyo walimtembelea Kamanda huyo katika kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma mara baada ya kuhitimisha matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.