Habari za Punde

Waliochukua Ubingwa wa ROLLING STONE Mwaka Jana Mjini Unguja Kuwapa Mazoezi Ndugu Zao Kombaini Mpya ya Mwaka Huu Kwa Kucheza Mchezo Maalum wa Kirafiki.

 Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Mabingwa wa mwaka jana katika Mashindano ya Vijana ya Afrika Mashariki na Kati (Rolling Stone) Timu ya Mjini Unguja watacheza mchezo maalum wa kirafiki na ndugu zao ambao wamechaguliwa kuunda timu ya Mjini Unguja msimu huu itakayokwenda kucheza Mashindano hayo mwezi July mwaka huu jijini Arusha, mchezo huo utapigwa kesho Alhamis majira ya saa 10:00 za jioni katika Uwanja wa Amaan.

Mnamo tarehe 9 July, 2016 siku ya Jumamosi timu hiyo ya Mjini Zanzibar ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Rolling stone kwa mara ya Kwanza ndani ya miaka 15 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya DAREDA ya Mkoani Manyara katika uwanja wa SHEIKH AMRI ABEID mjini Arusha.

Mabao ya Zanzibar Mjini siku hiyo yalifungwa na Ali Humud “Balii” dakika 42 na Hafidh Barik “Fii” dakika ya 44 huku bao pekee la DAREDA likifungwa na Najim Mussa dakika ya 83.
Timu hiyo ina Jumla ya wachezaji 22 ambao msimu huu wote wameachwa akibakishwa mmoja tu ambae ni Abdul rahman Juma “Baby” ambapo kesho watacheza mechi hiyo maalum na ndugu zao ambao msimu huu watakwenda wao kuwakilisha Zanzibar.

Kikosi hicho kilichobeba ubingwa kinaundwa na Walinda mlango Said Suleiman “De Gea” (Polisi) na Bashir Muslim “Iker” (Villa United-KVZ).Walinzi wa Pembeni: Abubakar Said “Riera” (Majimaji-Kijichi), Sadi Mgeni “King Sadi” (Kundemba-Kilimani City), Abdul hamid Salum “Ramos” (Charawe-KVZ) na Muharam Khamis “Terra” (Black Sailors).
Walinzi wa kati: Ali Humud “Balii” (Miembeni City-Jang’ombe Boys), Mwinjuma Mwinyi “Maggio” (Miembeni City-JKU) na Ibrahim Mohammed “Sangula” (Jangombe boys).

Viungo wachezeshaji: Fesal Salum “Fei toto” (JKU), Hassan Nassor “Abal” (Villa United), Amour Mundhihir “Mafisango” (Kwerekwe city- Charawe), Abdallah Mundhihir (Taifa Jang’ombe-Singida United) na Abdul Swamad Kassim (Jang’ombe boys).

Viungo washambuliaji: Abdul rahman Juma “Baby” (Villa Fc-KMKM), Suleiman Hassan “Kede” (KVZ), Ramadhan Khamis “Neymar” (Jangombe Boys) na Suwed Juma “ Aguero” (Polisi-JKU).

Washambuliaji: Yahya Hajj “Karoa” (Villa United-Miembeni City), Yunus Benard “Roma” (Villa United), Mohd Vuai “Prince” (Shangani-Miembeni City) na Hafidh Barik “Fii” (Jang’ombe boys).

Kwa upande wa Kikosi kipya cha Kombain ya Mjini ni:-
Walinda Mlango ni Rajab Farouk Festo (Real Kids), Peter Dotto Mashauri (Schalke 04) na Makame Mkadar Koyo (Huru). 
Wachezaji wa ndani ni Hassan Chalii (Kipanga), Abdul-halim Ameir (King Boys), Mahad Hassan Bai (Kijangwani), Yahya Silver (Muembe ladu), Shaaban Pandu (Villa United), Saleh Khatib (Kijangwani), Idrissa Makame (Villa FC), Ramadhan Simba (Calypso), Khatib Kombo (Schalke 04), Othman Jumbe (Black Sailors), Ali Hassan (Uhamiaji), Fahmi Salum (Mlandege), Salum Omar (Villa United), Yakoub Omar (Jang’ombe Boys), Nassir Ramadhan (Muembe Makumbi) na Mohd Ridhaa (Villa United).

Wengine ni Mussa Shaaban (Zimamoto), Ismail Kassim (Huru), Seif Said (KVZ), Abdillah Suleiman (King Boys), Haji Suleiman (JKU), Mohd Jailan (Chrisc), Makame Maoud (Schalke 04), Fahad Mussa (Mapembeani), Mohd Mussa (Mapembeani), Abrahman Juma (KMKM), Suleiman Dorado (Uhamiaji), Said Salum (Real Kids), Mohd Haji (Jang’ombe Boys), Abrahman Juma (ZAFSA), Abdul-hamid Juma (ZAFSA), Khatib Ameir (Real Kids), Yussuf Mohd (Muembe Beni) na Ibrahim Chafu (Villa FC).
Kwa upande wa viongozi wa timu hiyo ni wale wale ambapo kocha mkuu Mohammed Seif “King”, Kocha Msaidizi Ramadhan Abdul rahman “Madundo” ,  Mtunza Vifaa Nassir Kheir, Meneja wa timu Ali Othman “Kibichwa” na kocha wa Makipa Salum Ali “Chulas”.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.