Habari za Punde

Waziri wa Fedha Zanzibar Azungumza na Waandishi wa Habari Kuhusiana na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.

Waziri wa Fedha Zanzibar Dk Khalid Salum Mohd akizungumza na Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali vya Serikali na Binafsi muelekeo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018, inayotarajiwa kuwasilishwa katika Mkutano wa Sita wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, mkutano huo na waandishi umefanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha Vuga Zanzibar.Mjini Unguja.
Waziri wa Fedha Zanzibar Dk Khalid Salum Mohd akifafanua jambo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali Zanzibar Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar wakifuatilia kwa makini taarifa ya muelekeo wa Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mwaka 2017/2018 wakati akitowa maelezo hayo Waziri wa Fedha Zanzibar Dk Khalid Salum Mohammed katika ukumbi wa Wizara ya Fedha Vuga Zanzibar. 
Mwandishi wa habari wa Hit Fm Jaza Kombo akiuliza swali wakati wa mkutano huo na Waziri wa Fedha Zanzibar kuhusiana na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2017/2018.inatarajiwa kuwasilishwa katika Mkutano wa Sita wa Baraza la Wawakilishi wiki hii. 
Mwandishi wa Habari wa Habari Leo Khatib Suleiman akiuliza maswali kwa Waziri wa Fedha Zanzibar Dk Khalid Salum Mohd  alipozungumza na Waandishi kuhusiana na Mipango Mapendekezo ya Bajeti (Mapato na matumizi) ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017-2018.Katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha Vuga Mjini Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.