Habari za Punde

ZANTEL Kutoa Ofa Kwa Wateja Wake Kipindi cha Mfungo wa Mwezi wa Ramadhani

         
Wateja wa mtandao wa simu Zantel sasa kufurahia mawasiliano na ndugu jamaa na marafiki waliopo mashariki ya kati kwa bei nafuu kwa kutumia kifurushi cha kimataifa cha uarabuni.

Dar es Salaam, Mei 29 2017- Kampuni ya simu ya Zantel inaendelea kutimiza ahadi yake ya kuongeza thamani katika maisha ya wateja wao na sasa kutangaza ofa maalum inayowalenga waumini wa dini ya Kiislamu nchini ili kuadhimisha mwezi mtukufu wa mfungo wa Ramadhani duniani kote.

Akitangaza habari hii makao makuu ya kampuni ya Zantel yaliyopo Msasani jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Bw. Benoit Janin amesema “Ramadhani ni muda muafaka wa kujenga mahusiano mazuri na ndugu, jamaa na marafiki na ofa hii ni ishara ya Zantel kuwasaidia wateja wake kuweza kuungana na kuwasilia na kurahisiASHA zaidi na wapendwa wao”.
Aliongeza kwa kusema mtandao wa Zantel utaendelea kutoa huduma kwa mamilioni ya Watanzania kuwasaidia kutimiza malengo na ndoto zao kupitia vipengele mbali mbali vya huduma za kampuni hiyo ikiwa ni pamoja bidhaa na huduma za upigaji simu, vifurushi vya internet na mtandao.
 Alisema kampuni itahakikisha vyote hivi kwa kutoa huduma na bidhaa bora za upigaji simu na vifurushi vya intaneti huku tukihakikisha tunawekeza faida endelevu. Kwa mwaka 2016 kulikua na matatizo mbali mbali ila kwa sasa mkakati wetu ni kuhakikisha tunatoa vipaombele kwa vitu vyenye umuhimu mkubwa kwa wateja ikiwemo kuwa mtandao bora unaotoa intaneti ya kasi zaidi wa 4G, kupenya na kuwafikia watumiaji wengi zaidi, na kujiandaa kwa siku zijazo kuwa kampuni ya bidhaa inayopendwa zaidi.

“Tunahitaji kuwatayari kwa siku zijazo kwa njia mbali mbali za kuongeza mapato pamoja na huduma zinazoongeza thamani ya mtandao wa zantel ikiwemo uboreshaji wa vifurushi vya intaneti, tayari tunaona mabadiliko makubwa katika mtandao wetu ”aliongezea kwa kusema “Kutakua na bidhaa mbali mbali tutakazozitoa kipindi hiki zitakazofurahiwa na wateja wetu kukiwa na mpangilio wa ofa zilizoanza tarehe 24/05/2017”Aliongezea.
Akieleza zaidi kuhusu ofa hii, Mkurugenzi wa masoko wa Zantel Bw. Gasper Mbowa amesema” Ofa hii ya Ramadhani imelenga kuwazawadia wateja wetu wa malipo ya kabla watakaojiunga na vifurushi vyetu kwa kiasi chochote au kwa kuongeza muda wa maongezi kwenye kipindi cha mfungo wa Ramadhani. 

Mteja yoyote atakayeongeza muda wa maongezi atapata asilimia 50 ya muda wa maongezi moja kwa moja utakaomuwezesha kupiga simu Zantel kwenda Zantel, ofa hii itakua inatumika kuanzia saa 5 usiku hadi saa 12 asubuhi. 

Hivyo wateja wataweza kutumia huduma zetu zilizozinduliwa hivi karibuni kama ‘Zantel madrassa itakayowawezesha kujifunza dini ya kiislamu kwa kupokea mafunzo ya Quran, hadithi, dua, habari za BAKWATA na huduma nyingine nyingi kwa kupitia simu zao za mkononi kupitia ujumbe mfupi wa maneno au kwa kupiga simu.

Mbowa aliongezea kuwa wateja wa Zantel wanaweza kuwapigia simu ndugu, jamaa na marafiki waliopo mashariki ya kati kwa bei nafuu zaidi kupitia kifurushi cha kimataifa cha uarabuni. “Kwa shilingi za kitanzania 2,000 wateja watapatadakika 4 zakupigasimu  Qatar,Oman, UAE,Lebanon, Pakistan, Yemen& Saudi Arabia, nakwashilingi 5,000 watapatadakika 7kupigasimukwendakwenyenchitajwa, nafedhahizozitakatwamojakwamojakwenyeakauntizao”

Vifurushivyotehivivitapatikanakwakujiungakwakupiga*149*15#nakwavifurushivya‘BongaMpakabasi’, ‘Zantel Madrassa’ watejawatawezakujiungakwakutumaujumbewamanenokwakutumianeno SUBnakutumakwendanamba 15586 au kwakupiganamba 15586

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.