Habari za Punde

Balozi Seif Aifariji Familia ya Marehemu Dr. Karim Zam Ali.

Marehemu Dr. Karim Zam Ali amefariku dunia jana na kuzikwa leo katika kijiji chao cha Dimani Wilaya ya Magharibi B Unguja, wakati wa uhai wake aliwahi kuwa Afisa wa Kitengo cha Dawa za Usingizi   (Anaesthetist) ambae pia ni Mkufunzi wa Huduma ya kwanza katika Chuo cha Mwenge kiliopo Amani Mjini Zanzibar Dr. Karim Zam Ali aliyefariki Dunia Jana amezikwa Kijijini kwao Dimani Wilaya ya Magharibi “B”.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kati kati akiwafariji Wake wa Marehemu Dr. Karim Zam Ali alipofika Dimani kuwapa mkono wa pole  kufuatia Kifo cha Baba Watoto wao.Kushoto kwa Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi mheshimiwa Ayoub Mohamed Mahmoud.
Balozi Seif  Kushoto  akiifariji Familia ya Marehemu Dr. Karim  Zam Ali alipofika Kijiji kwao Dimani leo mchana kutoka mkono wa pole  kufuatia kifo cha mpendwa wao ambao aliwahi kuwa Daktari wa Michezo hapa Zanzibar.
Picha na – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.