Habari za Punde

Gari lapinduka na kujeruhi kadhaa kisiwani PembaGari la abiria aina ya TOYOTA DYNA lenye namba za usajili Z 330 GX limeanguka na kujeruhi watu 8 akiwemo mama na mtoto. 

Ajali hiyo imetokea leo 7/6/2017 Kiuyu Minungwini. 

Gari hilo lilianguka mara baada ya kupinda kona ya Msufini likitokea Chake Chake kuelekea Wete.

 WANANCHI na watoa huduma katika Hospitali ya Chake Chake, wakimsaidia kumpeleka katika chumba cha XRAYS mmoja wa majeruhi wa ajali ya Gari iliyotokea Kiuyu Msufini Wilaya ya Wete Mkao wa Kaskazini Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 BAADHI ya Madaktari wa Hospitali ya Chake Chake wakimshona mmoja wa majeruhi wa ajali ya Gari ya Abiria, iliyotokea Kiuyu Msufini Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

MADAKTARI wa Hospitali ya Chake Chake wakimpatia huduma ya kwanza mmoja wa majeruhi, wa ajali ya abiria aliyeumia mguu baada ya kufikishwa hospitalini hapo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.