Habari za Punde

HIlika awapa somo wachezaji wa Unguja watakaokwenda UMISSETA Mwanza


Mchezaji wa Timu ya Zimamoto Ibrahim Hamad Hilika

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Mshambuliaji wa klabu ya Zimamoto ya Zanzibar Ibrahim Hamad Hilika amewataka wachezaji wa timu ya soka Kanda ya Unguja UMISSETA kujituma zaidi ili kufikia malengo yao waliyojiwekea.

Hilika ameyasema hayo Amani asubuhi ya leo wakati Wachezaji hao walipomaliza mazoezi ambapo amewapa elimu kubwa kuhusu soka ili wafanikiwe na watimize ndoto zao.

Amewataka kujituma katika Mashindano ya UMISSETA huko Mwanza na wacheze kwa malengo kwani Zanzibar kuna vipaji vingi sana.

“Munakwenda Mwanza ndugu zangu fursa kubwa sana mumepata, angalieni kuna wachezaji wangapi hawajachaguliwa mumechaguliwa nyinyi, hivyo mujuwe kuwa nyinyi mumeaminiwa mukapigane na mukaoneshe vipaji vyenu kwani sisi Zanzibar tunavipaji vingi sana, mpira sasa ni ajira, mfano mimi nina mke wangu na kazi yangu nimepata kwaajili ya mpira, nauthamini na naupenda kwa vile ndio kazi yangu, ningekuwa sijajituma kucheza mpira si ningekuwa pengine sina lolote nakaa masikani tu, sasa nyinyi kachezeni kwa kufata mafunzo na ushauri wa walimu wenu, kwasababu nidhamu ndio siri ya mafanikio, wekeni malengo soka ni ajira sasa, si mumesikia kuwa Zanzibar imepata uanachama wa CAF!, sasa fursa hizo jamani, mimi nipo pamoja na nyinyi ndugu zangu, tutakufatilieni na tutafurahi sana mukibeba ubingwa, nakutakieni safari njema yenye mafanikio”. Alisema Hilika.

Mashindano ya UMISSETA yanayotarajiwa kuanza June 6, 2017 huko Chuo cha Ualimu Butimba Mkoani Mwanza ambapo kwa mwaka huu Zanzibar itashiriki kanda mbili tofauti, yani Kanda ya Unguja na Kanda ya Pemba.

Wachezaji 21 waliyochaguliwa kwenye kikosi hicho kinachotarajiwa kuondoka Visiwani Zanzibar siku ya Jumamosi ya June 3, 2017 ni :-.

WALINDA MLANGO
Aley Ali Suleiman (Ubago) na Ali Makame (Muembe ladu)

WALINZI
Ibrahim Abdallah Hamad (Arahman), Abdurahman Seif Bausi (Glorious), Abubakar Khamis (Bububu), Abdul aziz Ameir Khatib (Arahman), Ali Issa Omar (Lumumba),  Ahmed Mohd Shaaban (Nyuki) na Abbas Yahya.

VIUNGO
Amani Ali Suleiman (Kiembe Samaki), Ibrahim Faraj “Mess” (Lumumba), Haji Suleiman (JKU Mtoni), Yakoub Kiparo (Langoni), Jamali Ali Jaku “Ozil” (Kinuni) na Eliyasa Suleiman (K-pura).

WASHAMBULIAJI
Faki Kombo (JKU Mtoni), Mundhir Abdallah (JKU Mtoni), Ali Hassan (Bububu), Walid Abdi “Pato” (Mwera), Ali Mohd Seif (Tumekuja) na Ali Omar (Mwera).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.