Habari za Punde

Naibu Waziri OMPR afanya ziara kukagua maeneo yaliyoathirika na mvua za Masika kisiwani Pemba

 Ofisa Mdhamini Wizara ya Miundombinu , Mawasiliano na Usafirishaji Pemba, Hamad Ahmed Baucha, akitowa maelezo kwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa pili wa Rais Zanzibar, Mihayo Juma Nunga, juu ya uharibifu uliotokea katika bara bara ya Mkoani Pemba kufuatia Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.
 Baadhi ya Nyumba , ya Mwananchi ilivyoathirika kwa mvua kubwa inayoendelea kunyesha huko katika kijiji cha Mwambe Mkoani Pemba.
 Naibu waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wa pili wa Rais Zanzibar, Mihayo Juma Nunga, akimuelekeza neno Sheha wa shehia ya Mwambe Mkoani Pemba, baada ya naibu huyo kufanya ziara ya kukaguwa maeneo yaliothiriwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.
 Miongoni mwa muathirika wa maafa ya mvua akitowa maelezo kwa Naibu Waziri wanchi Ofisi ya Makamo wa pili wa Rais Zanzibar. Mihayo Juma Nunga, juu ya maafa hayo yalivyo muathiri huko katika kijiji cha Chonga Chake Chake Pemba.
 Muathirika mwengine wa maafa ya Mvua zinaendelea kunyesha, huko katika kijiji cha Uwandani Chake Chake , akitowa maelezo kwa Naobu Waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wa pili wa Rais Zanzibar, Mihayo Juma Nunga .baada ya kutembelea eneo hilo.


Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wa pili wa Rais Zanzibar, Mihayo Juma Nunga, akiangalia eneo la bara bara ya  Mchanga wa Kwale , namna ilivyoathiriwa na Mvua kubwa zinazoendelea Kunyesha.


Picha na  SAID ABDULRAHMAN- PEMBA.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.