Habari za Punde

Mazishi ya muasisi na mwanasiasa mkongwe Mzee Khamis Juma Mkadara


  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wa Tatu kutoka Kulia akijumuika pamoja na Viongozi na Wananchi katika kumsalia Mwanasiasa Mkongwe wa Kisiwani Pemba Mzee Khamis Juma Mkadara kwenye Msikiti wa Ijumaa Wawi Chake chake Pemba.


Kushoto ya Balozi Seif ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Juma Abdulla Juma {Mabodi } na kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Kilimo, Mali Asili, Mifugo na Uvuvi Mh. Hamad Rashid Mohamed.

Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mtaa wa Wawi Chake chake wakiwa miongoni mwa wananchi waliomsalia Kiongozi huyo nguli wa Kisiasa Kisiwani Pemba Mzee Mkadara.

 MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, akiwaongoza wananchi mbali mbali Kisiwani Pemba na Viongozi wa Serikali, katika mazishi ya Mwasisi wa Afro Shirazi Mrehemu Khamis Juma Mkadara aliyefariki Dunia Wawi Wilaya ya Chake Chake Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)


 Balozi Seif akimimina mchanga katika Kaburi la Mzee Khamis Juma Mkadara aliyezikwa katika Mavani ya Familia yake yaliyopo Mashariki ya Msiku wa Ijumaa wa Wawi Chake chake.
NAIBU katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mhe:Abdalla Juma Mabodi, akitia mchanga katika kabauri la mwasisi wa Afro Shirazi Marehemu Khamis Juma Mkadara, aliyefariki dunia na kuzikwa Wawi Wilaya ya Chake Chake Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

  

MWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Mkoani Abdalla Yussuf Ali, akisoma wasifu wa marhemu Mzee Khamis Juma Mkadara, mbele ya viongozi mbali mbali wa Serikali baada ya kumaliza mazishi yam zee huyo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar  Dr. Juma Abdulla Mabodi wa Pili kutoka Kulia akiwataka kuwa na moyo wa subra Wajukuu wa Mzee Mkadara.


Picha na – OMPR – ZNZ

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.