Habari za Punde

UANACHAMA WA CAF UNAENDELEA KUFANYA KAZI ZAKE, TIMU ZA BEACH SOKA ZAPEWA MASHARTI

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Vilabu vya soka la ufukweni Zanzibar vilivyo shiriki ligi kuu msimu uliopita vimepewa mwezi mmoja kuonana na mrajisi wa vyama vya michezo ili kusajiliwa rasmi.

Akizungumza na Mtandao huu Fahad Khamis Said ambae ni katibu wa kamati ya soka la ufukweni Zanzibar amesema vilabu hivyo wamevipa mwezi mmoja vikafanyiwe uhakiki kwa mrajis.

Akisisitiza katibu huyo amesema timu yoyote ambayo haitaenda kwa mrajis kuhakikiwa haitashiriki ligi kuu ya mchezo huo ambayo inatarajiwa kuanza mwezi wa July mwaka huu  kwenye fukwe za Bububu Bambuu ambapo amesema kwakuwa Zanzibar imepata uanachama wa CAF hawanabudi kufuta taratibu zote zilizokuwepo ili waendeshe kwa ufanisi zaidi soka lao.

''Tumepata uanachama wa CAF kwaiyo kila kitu kiende kwa utaratibu ikiwa timu haikwendwa kwa mrajis haitoshiriki ligi kuu msimu huu, bora tuwe na vilabu saba lakini vimesajiliwa''. Alisema Fahad.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.