Habari za Punde

HAPATOSHI 4 BORA REAL KIDS, FC MUEMBE BENI, SCHALKE 04 NA KING BOYS NANI BINGWA WA CENTRAL WILAYA YA MJINI MWAKA HUU?

Na:Abubakar.Khatib Kisandu, Zanzibar.
Hatua ya nne bora ligi za madaraja ya Vijana ndani ya Wilaya ya Mjini kwa upande wa daraja la Central inatarajiwa kuanza Jumamosi July 8, 2017 kwenye dimba la Amaan.

Akizungumza na Mtandao huu msemaji wa kamati ya Central Wilaya hiyo Mussa Habibu “Mzirai” amesema tayari timu 4 zimeshapatikana ambazo ni bingwa mtetezi FC Muembe beni, Real Kids, Schalke 04 na King Boys huku mchezo wa kwanza utapigwa kati ya King Boys dhidi ya Muembe beni saa 4:00 za asubuhi.

Amesema mchezo wa pili utapigwa Jumapili July 9, 2017 saa 4:00 za asubuhi kati ya Real Kids dhidi ya Schalke 04.

Kwa hatua nyengine Mzirai ameviomba vilabu hivyo kujiandaa vizuri katika hatua hiyo kwani ni ngumu sana na kila timu itapata matokeo kutokana na uwezo wao kwani kamati imejipanga kuhakikisha ligi hiyo inakuwa bora.

“Sisi kama kamati tumejipanga ili ligi iwe bora na kuvuta hisia za mashabiki kwani huku ndiko kunakotoka vipaji”. Alisema Mzirai.

Pia Mzirai ameziomba Kampuni, Mashirika ya UMMA na watu binafsi kujitokeza kuidhamini ligi hiyo kwa kuwapa zawadi na wao wapo tayari kufanya biashara na Kampuni yoyote kwani mpaka sasa hawajajua zawadi za washindi wa Mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.