Habari za Punde

Rais wa Tanzania Dkt. Magufuli Awasili Mkoani Mwanza na Awasalimia Wakazi wa Kona ya Bwiru Ghana na Aingia Kukagua Uwanja wa Nyamagana.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza kwa ziara ya siku mbili mkoani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Viongozi wa Dini mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza leo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia ngoma za asili kutoka katika kikundi cha Bujora mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiombewa sala na Viongozi mbali mbali wa dini kutoka Kanda ya ziwa mara baada ya kuwasili mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Kona ya bwiru katika barabara ya Airport wakati akitokea uwanja wa ndege wa Mwanza.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinunua Karanga kutoka kwa Mmachinga anayefanya biashara katikati ya jiji la Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa katikati ya jiji la Mwanza wakati akielekea Uwanja wa Nyamagana kuangalia mechi kati ya Buhongwa United naTimu ya Nyamwaga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa jiji la Mwanza wakati akielekea Uwanja wa Nyamagana kuangalia mechi kati ya Buhongwa United na Timu ya Nyamwaga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa jiji la Mwanza wakati akielekea Uwanja wa Nyamaga na kuangalia mechi kati ya Buhongwa United na Timu ya Nyamwaga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Buhongwa Fc mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Nyamagana. Jijini Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mpira pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongela katika uwanja wa Nyamagana ambapo timu ya Buhongwa United ilikuwa ikicheza na Nyamwaga FC.
 (Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.