Habari za Punde

Jumuiya ya Maendeleo ya Elimu Zanzibar (ZEDO) yawakutanisha wanachama wa Kijani kibichi wa Mkoa wa Kaskazini na Mkoa Kusini Unguja

 MWENYEKITI wa Jumuiya ya Maendeleo ya Elimu Zanzibar (ZEDO) ambae pia ni Mkurugenzi wa Mtandao wa Kijani kibichi Ussi Said Suleiman, akizungumza na wanachama wa mtandao huo wa Mkoa Kaskazini na Kusini kwa lengo la kuanzisha Kijiji kitakachozalisha zaidi ya ajira 2000.
 BAADHI ya wanachama wa Mtandao wa Kijani kibichi wa Mkoa wa Kaskazini na Kusini Unguja wakimsikiliza Mkurugenzi wa Mtandao huo Ussi Said Suleiman (hayupo pichani) katika mkutano uliofanyika Ofisi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Elimu Mikunguni mjini Zanzibar.

  MMOJa wa wanachama wa mtandao wa Kijani kibichi Bi. Eunice Peter akichangia katika mkutano wa kujadili maendeleo ya jumuiya hiyo.
WANACHAMA  wa Jumuiya ya ZEDO kutoka mikoa miwili ya Unguja, Kaskazini na Kusini waliohitimu mafunzo ya ujasiriamali wakiwa katika picha ya pamoja. Katikati ni Ussi Said Suleiman, Mwenyekiti wa jumuiya hiyo.

Picha na Makame Mshenga.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.