Habari za Punde

Timu ya JKU Yaipeleka Mchakamchaka Timu ya Kizimbani Kwa Ushindi wa Bao 7-2, Na Kulerea Kuongoza Ligi Hiyo.Huku Zimamoto Yaichapa Mwenge 3-1.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Timu ya Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar (JKU) imefanikiwa kuondoka na kapu la mabao kufuatia kuichapa Kizimbani mabao 7-2 katika mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora uliosukumwa jioni ya leo katika Dimba la Gombani Kisiwani Pemba.

Mabao ya JKU yamefungwa na Khamis Said dakika ya 37, 45,63 Amour Omar dakika ya 19, Muhammed Said Mpopo dakika ya 80,90 na Issa Haidar “Mwalala” dakika ya 89 kwa shuti kali kutoka katikati ya uwanja hadi goli,  huku mabao ya kufutia machozi ya Kizimbani yote yamefungwa na Nassir Suleiman dakika ya 50 na 73.

Mchezo mwengine leo umepigwa katika dimba la Amaan ambapo Zimamoto wakaichapa Mwenge mabao 3-1.

Mabao ya Zimamoto yamefungwa na Ibrahim Hamad Hilika dakika ya 12 na Nyange Othman Denge dakika ya54 na 61 ambapo bao pekee la Mwenge limefungwa na Sharifu Hamad dakika ya 69.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa kupigwa michezo 2 katika viwanja viwili tofauti majira ya saa 10:00 za jioni.

Katika uwanja wa Amaan watasukumana kati ya Jang’ombe boys dhidi ya Okapi na katika uwanja wa Gombani Jamhuri watakipiga na Taifa ya Jang’ombe.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.