Habari za Punde

Wafanyakazi wa Vyama Vya Wafanyakazi Wapata Mafunzo ya Kisheria Pemba.

MRATIBU wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Fatma Khamis Hemed, akielezea kazi na malengo ya kituo hicho, kabla ya kuanza kwa mafunzo ya haki za binadamu kwa wafanayakazi wa vyama vya wafanyakazi kisiwani Pemba, mafunzo hayo yalifanyika ofisi ya ZLSC mjini Chakechake 
KATIBU tawala wilaya ya Micheweni kisiwani Pemba, Hassan  Abdalla Rashid, akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wanachama wa vyama vya wafanyakazi kisiwani kisiwani humo, mafunzo hayo yameandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, na kufanyika ofisini kwao mjini Chakechake
AFISA Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanziba ZLSC tawi la Pemba, Siti Habib Mohamed, akitoa mada ya sheria ya uajiri no 11 ya mwaka 2005, kwa wanachama na viongozi wa vyama vya wafanyakazi kisiwani humo, mafunzo hayo yameandaliwa na kufanyika ofisi ya ZLSC  mjini Chakechake
WANACHAMA wa vyama mbali mbali vya wafanayazi kisiwani Pemba, waliohudhuria mafunzo ya haki za binadamu, yalioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, na kufanyika ofisi ya ZLSC mjini Chakechake.
WANACHAMA wa vyama mbali mbali vya wafanayazi kisiwani Pemba, waliohudhuria mafunzo ya haki za binadamu, yalioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, na kufanyika ofisi ya ZLSC mjini Chakechake, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.