Habari za Punde

Zimamoto na Jamuhuri Zagombea Nafasi ya Kushiri Kombe la Shirikisho Afrika Wapishana Kwa Point 1.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Bingwa mpya wa ligi kuu soka ya Zanzibar kwa msimu wa mwaka 2016-2017 tayari ameshapatikana ambae ni JKU huku akiwa amebakiwa mchezo mmoja mkononi dhidi ya Mwenge utakaopigwa Jumamosi ya Agost 19, 2017 katika uwanja wa Amaan.

Lakini homa kali katika ligi hiyo ni nani atamaliza nafasi ya pili kati ya Zimamoto yenye alama 25 au Jamhuri yenye points 24 ambapo wote wamebakiwa na mchezo mmoja mkononi.

Kwa mujibu wa ratiba Zimamoto atamalizana na Kizimbani wakati Jamhuri watakipiga na Jang’ombe Boys ambapo michezo hiyo ilikuwa imepangwa siku tofauti katika uwanja wa Gombani yani Jumamosi na Jumapili lakini kutokana na umuhimu wa michezo hiyo ZFA imelazimika michezo hiyo kuipanga siku moja na wakati mmoja ili kuepusha upangaji wa matokeo.

Bingwa na Makamo Bingwa wa ligi hiyo watawakilisha Zanzibar katika Mashindano ya Kombe la Klabu Bingwa pamoja na Kombe la Shirikisho Barani Afrika ambapo msimu uliopita waliwakilisha Zimamoto na KVZ ambao wote walitolewa mzunguko wa kwanza.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.