Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akibadilishana
nyaraka na Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) nchini Tanzania,
Chansa Kapaya (kulia) zenye makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi
wa Burundi wanaohifadhiwa mkoani Kigoma.Makubaliano hayo yamefanyika mwishoni
mwa wiki, Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, jijini Dar es
Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani na Elimu ya Uzalendo kutoka nchini Burundi,
Pascal Barandagiye, akibadilishana nyaraka na Mwakilishi wa Shirika la
Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) nchini Tanzania, Chansa Kapaya (kulia)
zenye makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi
wanaohifadhiwa mkoani Kigoma.Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mwigulu Nchemba.Makubaliano hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki, Ukumbi wa
Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke, akifafanua
vipengele vilivyopo kwenye Mpango wa
Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa mkoani Kigoma, kabla ya kutiwa
saini.Wanaosikiliza meza kuu toka kushoto ni
Waziri wa Mambo ya Ndani na Elimu ya Uzalendo kutoka nchini Burundi,
Pascal Barandagiye, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba,
Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) nchini Tanzania,
Chansa Kapaya na Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR)
nchini Burundi,Abel Mbilinyi.Makubaliano hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki,
Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam
Wajumbe kutoka Serikali ya Burundi wakiongozwa na Balozi wa Burundi
nchini Tanzania,Gervais Abayeho wakiwa katika Mkutano wa makubaliano juu ya Mpango
wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa mkoani Kigoma.Makubaliano
hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki,Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius
Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Wajumbe kutoka Mashirika
mbalimbali ya kimataifa wakiwa katika Mkutano wa makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi
wanaohifadhiwa mkoani Kigoma.Makubaliano hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki, Ukumbi
wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment