Habari za Punde

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mpango Ayataka Mabenki Kuongoza Ubunifu Ili Kuchochea Uchumi.


Waziri wa Fedha na Mipango Mh. Dk. Philip Mpango akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa uuzaji hisa za Maendeleo Bank PLC. Pamoja nae kutoka kushoto ni Askofu Ambele Mwaipopo, Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Askofu Dk. Alex Malasusa, Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Bw. Ibrahim Mwangalaba na Mwenyekiti wa Bodi ya Maendeleo Bank Bw. Amulike Ngeliama. 

Waziri wa Fedha na Mipango Mh. Dk. Philip Mpango akizungumza na wageni waalikwa jana katika hafla ya uzinduzi rasmi wa uuzaji hisa za Maendeleo Bank PLC uliofanyika jijini Dar esSalaam.
Wakati Maendeleo Bank ikiwa ni taasisi ya nane ya fedha kuorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Serikali imesema asilimia 60 ya miamala ya fedha nchini haipiti kwenye mifumo rasmi.
Hivyo, benki na taasisi za fedha zimetakiwa kuongeza ubunifu ili sekta hiyo iweze kuchochea maendeleo ya uchumi. Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango wakati wa hafla ya uzinduzi wa uuzaji wa hisa za Maendeleo Bank PLC na kwamba, kwa sasa ni asilimia 40 tu ya miamala ya fedha hupita katika mifumo rasmi.
Maendeleo Bank inakuwa benki ya kwanza kuhitimu kutoka dirisha la ukuzaji mashirika machanga (Enterprise Growth Market) na mwaka 2016 ilipata tuzo ya kampuni bora katika makampuni yanayokua kutoka Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).
Dk. Mpango alisema sekta ya benki ni muhimu katika kukuza uchumi na kwamba, kupitia huduma za fedha kwa kutumia simu za mikononi, Tanzania ni kati ya nchi zinzoongoza Afrika kwa kusogeza karibu huduma za kibenki kwa wananchi.. “Kwa hili Benki ya Maendeleo lazima muongeze ubunifu ili kuvutia wateja zaidi kutumia huduma zenu,” Dk. Mpango alitaka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) kuongeza nguvu ya kuelimisha jamii umuhimu wa umiliki wa hisa.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank, Ibrahim Mwangalaba alisema, tangu benki ianzishwe mwaka 2013 imekuwa namafanikio makubwa ikiwamo kuongeza matawi kufikia matatu.
Mwangalaba alisema mwaka 2015, benki ilipata faida ya Sh. 175 milioni na mwaka 2016 iliongezeka na kufikia Sh. 555 milioni. Pia, kwa miaka minne imelipa kodi ya Sh. 2.42 bilioni.
Ailongeza kuwa mwaka 201/16, benki ilipata kibali cha kuuza hisa stahili na ilikusanya zaidi ya Sh. 2.8 bilioni, hivyo kufikisha jumla ya Sh. 7.30 bilioni.“Leo tunashuhudia uzinduzi wa uuzaji wa hisa ukiwa na lengo la kuongeza mtaji kwa Sh. 15 bilioni, ambazo zitatumika kuimarisha shughuli za uendeshaji,” alisema.Tangu benki ianzishwe imefanikiwa kukusanya amana zaidi ya Sh. 39 milioni na kutoa mikopo zaidi ya Sh. 28.0 milioni. Pia, mali za benki zina thamani ya Sh. 49 bilioni.Mwangalaba alisema iwapo watafanikiwa kuuza hisa na kupata ntji wa Sh. 15 bilioni, wanatarajia kuimarisha utendaji wa benki hiyo kwa kiwango kikubwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.