Habari za Punde

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Mohammed Aboud Alitaka Jeshi la Polisi Zanzibar Kuzidisha Kasi Katika Kupambana na Biashara ya Dawa za Kulevya Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akisalimiana na Kaimu Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibat Juma Yussuf alipowasili katika majengo ya Makao Makuu ya Polisi Kilimani Zanzibar kwa ziara ya kikazi kutembelea Jeshi la Polisi Zanzibar.  
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akisalimiana na Makamanda wa Jeshi la Polisi Zanzibar alipowasili katika viwanja vya Makao Makuu ya Polizi Kilimani Zanzibar kwa ziara ya kikazi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akisalimiana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Hassan Nassir alipowasili katika viwanja vya  majengo ya Makao Makuu ya Polisi Kilimani Zanzibar akiwa katika ziara ya kikazi. 
Makamanda wa Jeshi la Polishi Zanzibar wakitowa heshima na kuimba wimbo wa utii wa Jeshi la Polisi wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohammed Aboud Mohammed wakiwa katika ukumbi wa mkutano katika majengo ya Makao Makuu wa Jeshi la Polisi Kilimani Zanzibar. 
Kaimu Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Juma Yussuf akitowa taarifa ya utendaji wa Jeshi hilo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohammed Aboud Mohammed wakati wa ziara yake kutembelea na kupata taarifa za utendaji wa kazi ya jeshi hilo Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akizungumza na Makamanda wa Jeshi la Polishi Zanzibar wakati wa mkutano wake na maofisa hao uliofanyika katika ukumbi wa Makao Makuu ya Polisi Kilimani Zanzibar. Na kuwataka kuendelea jitihada katika kupambana na Biashara ya Dawa za Kulevya Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Maofisa wa Jeshi la Polishi Zanzibar akiwa katika ziara yake kutembelea sehemu mbalimbali kujionea utendaji wa kazi wa taasisi hizo. 
Waandishi wa habari na Maofisa wa Polisi wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakifuatilia mkutano huo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe Mohammed Aboud Mohammed.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.