Habari za Punde

WIKI YA JANG'OMBE BOYS HAPATOSHI, YAANZA RASMI LEO KWA KUFUNGUA MATAWI

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Timu ya Jang'ombe Boys inayoshiriki ligi kuu soka ya Zanzibar imeanzisha wiki yao maalum kuanzia leo Alhamis ya Septemba 7 mpaka 10, 2017 kwa kufanya shughuli mbali mbali zikiwemo za kijamii pia.

Zoezi hilo linasimamiwa na uongozi wa Friends of Boys chini ya katibu wake Alawi Haidar Foum ambapo amesema wameanzisha wiki hiyo kwa ajili ya kuzidi kukaa karibu na jamii ya Kizanzibar.

"Sisi kama Jang'ombe boys kupitia  Friends of Boys tumeanzisha wiki hii kwa kujiweka karibu na wadau wetu, tutazidi kufungua matawi, tutafanya usafi wa Mazingira, tutafanya harambee ya utambulisho na mwisho tutacheza mechi ya kirafiki" Alisema Alawi.

RATIBA KAMILI HII HAPA YA WIKI YA BOYS
07/09/2017. KUFUNGUWA MATAWI.
08/09/2017. USAFI WA MAZINGIRA.
09/09/2017. HARAMBEE UTAMBULISHO.
10/09/2017. MECHI YA KIRAFIKI.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.