Habari za Punde

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombo Azungumza na Madaktari Kutoka ( WAMY)

Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo kulia akimkabidhi cheti Dk,Ahmed Yasin Abukrecha ambae ni miongoni mwa madaktari kutoka Jumuiya ya Vijana wa Kiislam Duniani(WAMY)waliofanya Matibabu kisiwani Pemba katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Mjini Unguja.
Kiongozi wa  Madaktari kutoka Jumuiya ya Vijana wa Kiislamu Duniani(WAMY) Dk,Sultan Baghdadi akizungumza machache kuhusiana na Matibabu walioyafanya kisiwani Pemba katika mkutano na Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Mjini Unguja.
 Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na Madaktari kutoka Jumuiya ya Vijana wa Kiislamu Duniani(WAMY) kuhusiana na Matibabu walioyafanya kisiwani Pemba katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Mjini Unguja.
Mkurugenzi Idara ya Huduma za Hospitali Wizara ya Afya Zanzibar Dk,Mohammed Dahoma akitoa neno la shukurani kwa Madaktari kutoka Jumuiya ya Vijana wa Kiislamu Duniani(WAMY) kuhusiana na Matibabu walioyafanya kisiwani Pemba katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Mjini Unguja.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.