Habari za Punde

Balozi Seif akagua maeneo yaliyoathirika na mafuriko

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akifanya ziara ya kukagua maeneo yaliyoathirika na Mvua za Vuli katika Shehia ya Kijichi Wilaya ya Magharibi”A”.
 Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “A” Kepteni Khatib Khamis wa kwanza kutoka Kushoto akimpatia maeleza Balozi Seif  juu ya maafa ya mabvua za Masika zilizoathiri Shehia ya KIjichi.

 Balozi Seif akiuagiza Uongozi wa Wilaya ya Magharibi A kusimamia sheria na taratibu dhidi ya watu wanaoamua kujenga bila ya kuzingatia Sheria zilizowekwa.
  Kasi ya maji ya mvua yanayoonekana yakititirika katika Mto wa Bububu kutokana na baadhi ya Watu wengi kutozingatia njia za maji hayo kutokana na ujenzi holela.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizipa pole Fmilia mbili zilizooondokewa na Jamaa zao kufuatia mafuriko ya mvua za Vuli zilizonyesha Juzi.

Na Othman Khamis OMPR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alionya kwamba katika utaratibu wa kunusuru Maafa hasa kwenye  maeneo hatarishi  Serikali Kuu italazimika kuvunja majengo yote yaliyojengwa bila ya kuzingatia  sheria za ujenzi zilizowekwa.

Alisema baadhi ya nyumba zisizozingatia Mfumo wa Mipango Miji, Mamlaka zinazosimamia Ujenzi zitalazimika kuchukuwa hatua dhidi ya watu wote waliojenga bila ya kupata vibali kutoka Mamlaka hizo.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa agizo hilo alipofanya ziafa fupi ya kuzipa pole familia za Watu waliofiwa na jama zao pamoja na kukagua maeneo yaliyoathariki kutokana na maafa ya mafuriko ya Mvua za Vuli katika Shehia ya Bububu Kijichi Wilaya ya Magharibi “A”.

Alisema wakati umefika kwa Jamii kulazimika kufuata Sheria za Nchi na kuacha tabia ya muhali ambayo kwa kiasi kikubwa tayari imeshaathiri Jamii kwa kiasi kikubwa katika masuala mbali mbali likiwemo lile sugu lililoshamiri hivi sasa la ushalilishaji wa Kijinsia.

Balozi Seif alitahadharisha wazi kwamba  Wananchi wasipozingatia taratibu za Nchi hata zile za Dini pamoja na Kimila Jamii itaelekea mahali pabaya pa maangamizi na ni vyema hali hiyo ikapaswa kutafutiwa dawa ya haraka.

Katika ziara hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alitoa Mkono wa pole kwa Familia ya Bwana Hussein Khamis Hamad aliyefiwa na Mama yake Mzazi Marehemu Bibi Salma Khamis na Bwana Rajab Moh’d aliyeondokewa na Mtoto wake.

Balozi Seif  alizitaka Familia hizo kuwa na moyo wa subra katika kipindi hichi kigumu cha  msiba wa wapendwa wao na wanapaswa kukubali kuwa matukio hayo ni kudra za Mwenyezi Muungu.

Mapema Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “A” Kepteni Khatib Khamis  alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba  sababu kubwa iliyopelekea maeneo ya Bubu Kijichi kukumbwa na mafuriko ya maji kunatokana na baadhi ya Watu kutozingatia utaratibu wa Ujenzi.

Kepteni Khatib alisema baadhi ya Watu wameshindwa kufuata Sheria za Ujenzi licha ya kwamba Viwanja walivyopewa vilipata baraka ya upimwaji halali na hatimae  kuvuruga Mipango hiyo.

Alisema zipo nyumba zilizojengwa katika vianzio vya Maji na nyengine zimetiwa kuta ndani ya mitaro ya mito ya maji kitendo ambacho kimezalisha maafa yanayoweza kuepukwa mapema.

Alifahamisha kwamba kasi ya maporomoko ya maji itaongezeka na maafa yataendelea kushuhudiwa iwapo wajenzi holela katika maeneo yao hawatadhibitiwa mapema.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.