Habari za Punde

ZURA yatangaza bei mpya ya mafuta

 Kaimu Mkurugenzi Huduma Kwa Wateja Zanzibar Mussa Ramadhani Haji akizungumza na waandishi huko Ofisini Maisara. Picha na Kijakazi Abdallah

Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa huduma kwa wateja ( hayupo pichani) Picha na Kijakazi Abdallah

Mwashungi Tahir  Malezo Zanzibar       

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma nishati na Maji Zanzibar  ZURA imesema bei mpya ya mafuta ya Dizeli na Mafuta ya taa katika mwezi wa Novemba 2017 zimepanda ikilinganishwa na bei za bidhaa hizo katika mwezi wa Oktoba 

Akizungumza na waandishi wa Habari huko katika ofisi yao ilioko Maisara Kaimu Mkurugenzi Huduma Kwa Wateja Zanzibar Mussa Ramadhani Haji wakati alipokuwa akitoa taarifa juu ya mabadiliko ya bei mpya za mafuta ambazo zitaanza kutumia hapo kesho 8/11/2017.

Alisema kuwa kupanda kwa bei za mafuta hapa Zanzibar kumetokana na kupanda kwa wastani kwa bei katika soko la Dunia na kupanda kwa gharama za usafirishaji , Bima kwa Petrol zimepanda kwa shilingi 21.73 sawa na asilimia 11%, kwa Dizeli imepanda kwa shilling 76.85 sawa na asilimia 29.4% na kwa mafuta ya taa zimepanda kwa shilling 18.7 sawa na asilimia 8.4%.

Aidha alisema bei ya rejareja ya mafuta ya Petrol kwa mwezi wa Novemba 2017  imeshuka  kwa shillingi 15 kwa lita kutoka shilling 2,145 kwa lita katika mwezi wa Oktoba 2017  hadi shillingi 2, 130 kwa lita katika mwezi wa Novemba 2017 sawa na asilimia 0.7%.

Pia alielezea bei ya reje reja ya mafuta ya Dizeli kwa mwezi wa Novemba 2017 imepanda kwa shillingi 190 kwa lita kutoka shilingi 2, 090 kwa lita katika mwezi wa Oktoba 2017 hadi shilingi 2,280 kwa lita katika mwezi Novemba 2017 sawa na asilimia 9%.

Vile vile alisema bei ya rejareja ya mafuta ya taa kwa mwezi Novemba 2017 imepanda kwa shilingi 25 kwa lita kutoka shilingi 1,514 kwa lita katika mwezi wa Oktoba 2017 hadi shilingi 1,539 kwa lita katika mwezi wa Novemba 2017 kwa ongezeko asilimia 2%.

Hata hivyo alisema bei ya reja reja ya Banka kwa mwezi  Novemba 2017 imepanda kwa shilingi 196 kwa lita kutoka shilingi 1,932 kwa lita katika mwezi Oktoba 2017  hadi shilingi 2,122 kwa lita katika mwezi wa Novemba 2017  sawa na ongezeko la asilimia 9%.

Vile vile Kaimu Mkurugenzi huyo amesema ( ZURA )imepanga bei hizo kwa kuzingatia wastani wa mwenendo wa mabadiliko ya bei za mafuta ya Dunia pamoja na thamani ya shilingi ya Tanzania ,gharama za usafiri ,bima ,kodi za Serikali na kiwango cha faida kwa wauzaji wa jumla na rejareja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.