Habari za Punde

Mabosi wa Kampuni wa inayojenga Uwanja wa Mao watinga Zanzibar, Sasa uwanja huo utakamilika Juni 2018Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo imepokea viongozi wakuu  wa kampuni ya Zhengtar Group Company Limited ya nchini China ambayo ndio inayojenga viwanja vya Michezo vya Mao Tse Tung.

Viongozi hao wamekutana na Waziri wa Wizara hiyo Rashid Ali Juma kufanya mazungumzo  na baadae kuangalia kazi za ujenzi wa viwanja hivyo unavyoendelea huko Mao Tse Tung .

Akizungumza na Waandishi wa Habari Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Omar Hassan “King” amesema kwa mujibu wa  viongozi  hao kazi ya ujenzi wa uwanja huo inatarajiwa kukamilika kama   makubaliano ya mkataba yalivoelekeza.

Amesema  kwa mujibu mkataba  baina ya kampuni  hiyo na wizara uwanja huo  ulikuwa ukamilike mwezi wa  tatu mwakani kwa kazi za awali   lakini kutokana na kuchelewa kwa vifaa vya ujenzi huo  unaweza kuchelewa kwa muda wa miezi  miwili hadi mitatu ya ziada.

Hata hivyo Kingi amesema  kutokana na hali ya haraka unavyokwenda ujenzi wa uwanja huo unatazamiwa utakamilika  mwezi wa June  hadi July  mwaka 2018.

 Uwanja huo utakuwa na Viwanja viwili vya mpira wa miguu na chengine cha michezo ya ndani kama vile Mpira wa Kikapu, Mpira wa Mikono, Mpira wa Pete na mengineyo.

Katika Viwanja hivyo vya Mpira wa Miguu uwanja mmoja utakuwepo upande wa Magharibi ambao utakuwa na Jukwaa moja litakalochukuwa Mashabiki 1500 waliokaa huku uwanja mwengine wa mpira wa miguu utakuwepo upande wa Mashariki ambao utakuwa na uwezo wa kuchukua Mashabiki waliokaa 900 katika jukwaa moja ambalo litakuwepo katika Uwanja huo, pia Viwanja hivyo vitakuwa na taa ambazo zitaweza kuwezesha kuchezwa michezo hadi usiku.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.