Habari za Punde

Maadhimisho ya Siku ya Wazazi Skuli ya Maandalizi Star Pemba.

Wanafunzi wa skuli ya Maandalizi ya star, iliopo Kichungwani wilaya ya Chakechake kisiwani Pemba, wakikaza meno kwenye mchezo wa kuvuta kamba, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za siku ya wazazi, iliofanyika uwanja wa Tenis Chakechake
Mwalimu Mkuu wa skuli ya Maandalizi ya star, iliopo Kichungwani, Chakechake Pemba, Moza Said, akisoma hutuba ya kumkaribisha mgeni rasmi, ambae ni aliewahi kuwa Mkuu wa wilaya ya Chakechake Hanuna Ibrahim Massoud, kwenye hafla ya siku ya wazazi, iliofanyika uwanja wa Tenis Chakechake
Aliekuwa Mkuu wa wilaya ya Chakechake Hanuna Ibrahim Massoud, akizungumza na wanafunzi, waalimu, wazazi na walezi wenye watoto wao skuli ya Maandalizi ya Kichungwani Chakechake, kwenye hafla ya sherehe ya siku ya wazazi, na kufanyika uwanja wa Tenis.
(Picha na Haji Nassor, Pemba)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.