Habari za Punde

KIKOSI CHA ZANZIBAR HEROES KINAENDELEA NA MAZOEZI

Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Kikosi cha timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kinaendelea na mazoezi yake kujiandaa na Mashindano ya CECAFA Chalenj CUP yanayotarajiwa kufanyika Novemba 25 na kumalizika Disemba 9, 2017 huko nchini Kenya.

Mazoezi hayo yanayosimamiwa na kocha mkuu wa kikosi hicho Hemed Suleiman (Morocco) yanaendelea kila siku kuanzia saa 2:00 za asubuhi katika uwanja wa Amaan Mjini Unguja.

Mpaka sasa wachezaji waliyoanza mazoezi ni wale ambao vilabu vyao vya Unguja huku ikiwa bado makundi mawili kutoka Kisiwani Pemba na Tanzania Bara bado hawajajumuika na wenzao ambapo wale kutoka Pemba wakitarajiwa kesho kuungana na wenzao.

Wachezaji waliyoanza mazoezi ni Walinda mlango Ahmed Ali "Salula" (Taifa ya Jang'ombe) na Mohammed Abdulrahman "Wawesha" (JKU), Walinzi Mohd Othman Mmanga (Polisi), Ibrahimm Mohammed "Sangula"(Jang'ombe Boys), Abubakar Ame "Luiz" (Mlandege), Issa Haidar "Mwalala" (JKU) na Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang'ombe).

Viungo Abdul-swamad Kassim (Miembeni City), Abdul Aziz Makame (Taifa ya Jang'ombe), Amour Suleiman "Pwina" (JKU), Hamad Mshamata (Chuoni) pamoja na washambuliaji Ali Badru (Taifa ya Jang'ombe)
Salum Songoro (KVZ), Khamis Mussa "Rais" (Jang'ombe boys) na Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto).

Ambao bado hawajawasili kutoka Pemba ni Mlinda mlango Nassor Mrisho (Okapi), Viungo Omar Juma "Zimbwe" (Chipukizi) na Mbarouk Marshed (Super Falcon) pamoja na mshambuliaji Mwalimu Mohd (Jamhuri).

Wachezaji ambao wanatokea ligi kuu soka Tanzania bara ambao bado hawajajumuika na wenzao ni Walinzi Abdallah Haji "Ninja" (Yanga), Adeyum Saleh "Machupa" (Kagera Sugar), Haji Mwinyi Ngwali (Yanga), Abdulla Kheir "Sebo" (Azam), Viungo Mudathir Yahya (Singida United), Mohd Issa "Banka" (Mtibwa Sugar) na Suleiman Kassim "Seleembe" (Majimaji) pamoja na washambuliaji Kassim Suleiman (Prisons), Matteo Anton (Yanga) na Seif Rashid Abdallah “Karihe” (Lipuli).

Kiungo mshambuliaji Feisal Salum (JKU) nae bado hajajiunga na wenzake kufuatia kuwepo kambi ya timu ya Taifa ya Vijana Tanzania wenye umri chini ya miaka 23 Kilimanjaro Warriors huku mshambuliaji Ali Yahya anaecheza soka nchini Spain nae bado hajawasili Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.