Habari za Punde

Mapinduzi Cup kuanza rasmi Ijumaa

Zijue timu 11 zitakazoshiriki 

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Pazia la Mashindano ya Kombe la Mapinduzi linatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake kesho kutwa Ijumaa Disemba 29, 2017 katika uwanja wa Amaan.

Siku hiyo itapigwa michezo mitatu ambapo saa 8:00 za mchana wataanza kati ya Mlandege dhidi ya JKU, Saa 10:00 za jioni Jamhuri watacheza na ndugu zao Mwenge na  saa 2:15 usiku Zimamoto watakipiga na Taifa ya Jang'ombe.

Jumla ya timu 11 zitakazoshiriki Mashindano hayo zikiwemo sita za Zanzibar, nne kutoka Tanzania bara na moja kutoka Uganda ambapo zimepangwa katika makundi mawili A na B.

Katika kundi A, kuna Mabingwa watetezi Azam FC, Simba SC, URA, Mwenge na Jamhuri. 

Katika michuano hiyo Klabu ya Yanga ambayo ipo katika kundi B, ipo pamoja na timu za Zimamoto, Mlandege, JKU, Taifa ya Jang'ombe na Singida United .

Ratiba kamili hii hapa.

Dec 29, 2017 Ijumaa saa 8:00 mchana Mlandege vs JKU  Group B, 
saa 10:00 Jamhuri vs  Mwenge Group A, 
saa 2:15 Zimamoto vs Taifa ya Jan’gombe Group B

Dec. 30, 2017 Jumamosi saa 10:00 Zimamoto  vs JKU  Group B, 
Saa 2:15 Taifa ya Jan’gombe vs Mlandege  Group B

Dec. 31,2017 Jumapili Saa 10:00 Azam    vs   Mwenge  Group A,
 saa 2:15 Jamhuri vs URA  Group A

Jan. 1, 2018 Jumatatu Saa 10:00 Mlandege  vs  Zimamoto  Group B, 
saa 2:15 JKU vs   Taifa ya Jan’gombe Group B

Jan. 2, 2018 Jumanne Saa 10:00 Singida united  vs Zimamoto Group B, 
saa 2:15 Simba    vs Mwenge Group A Yanga   vs   Mlandege Group B

Jan. 3, 2018 Jumatano URA vs   Mwenge Group A Azam   vs   Jamhuri Group A Taifa ya Jan’gombe vs Singida united Group B

Jan. 4, 2018 Thursday JKU    vs Yanga Group B
Simba    vs   Jamhuri Group A

Jan. 5, 2018 Friday Mlandege  vs  Singida united Group B URA    vs   Azam  Group A Yanga   vs  Taifa ya Jan’gombe  Group B

Jan. 6, 2018 Saturday JKU   vs  Singida united  Group B Simba    vs   Azam  Group A

Jan. 7, 2018 Sunday Zimamoto vs  Yanga  Group B

Jan. 8, 2018 Monday Simba    vs URA  Group A Yanga   vs  Singida united Group B

Jan. 9, 2018 Tuesday Mapumziko

Jan.10,2018 Wednesday 1st Semi Final (Winner Group A, Runners Up Group )

10:30 jioni 2nd Semi Final(Winner Group B, Runners Up GroupA)

2:15 usiku

Jan. 13, 2018 Saturday MAPINDUZI CUP FINAL 2018 8:00 pm (saa 2:00 usiku).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.