Habari za Punde

Shirika la Ndege la ACTL Air Tanzania Lafungua Ofisi Mpya Zanzibar.

 
Naibu Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mhe, Mohammed Abdalla Salum katikati akikata Utepe kuashiria Ufunguzi wa Ofisi mpya ya Shirika la Ndege la ACTL Air Tanzania Kijangwani Posta mjini Unguja.kushoto yake ni Naibu Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe,Chumu Kombo Khamis na Kulia ni -Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ndege la ACTL Ar Tanzania Eng Emanuel Koroso.
Katibu Mtendaji Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dk,Lila Vuai Lila kushoto na Kaimu Mkurugenzi Mkuu  wa Shirika la Ndege la ACTL Air Tanzania Albinus Manumbu wakitiliana saini mkataba wa utumiaji wa ndege kwa watalii watakaofika Zanzibar katika Ufunguzi wa  Ofisi yao Mpya Kijangwani Posta mjini Unguja.
Katibu Mtendaji Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dk,Lila Vuai Lila kushoto na Kaimu Mkurugenzi Mkuu  wa Shirika la Ndege la ACTL Air Tanzania Albinus Manumbu wakibadilishana hati ya  mkataba wa utumiaji wa ndege kwa watalii watakaofika Zanzibar katika Ufunguzi wa  Ofisi yao Mpya Kijangwani Posta mjini Unguja.
Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mhe,Mohammed Abdalla Salum akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Ofisi Mpya ya Shirika la Ndege la ACTL Air Tanzania Kijangwani Posta mjini Unguja.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ndege la ACTL Ar Tanzania Eng Emanuel Koroso akitoa hotuba ya makaribisho kwa Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Ofisi yao Mpya Kijangwani Posta mjini Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.