Habari za Punde

Zantel yakabidhi Majenereta kwa Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia

 Mkurugenzi wa Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia, Zanzibar Abdulhamid Idrissa Haji (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mjini Zanzibar mwishoni mwa juma wakati wa hafla ya kupokea majenerata matatu kutoka Zantel yatakayowasaidia wanafunzi wa chuo hicho katika masomo yao kama mbadala wa nishati hasa kipindi ambacho Umeme umekatika.
 Mkuu wa Zantel, Zanzibar Mohamed Mussa Baucha, akizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar mwishoni mwa juma wakati wa hafla ya kukabidhi majenerata matatu kwa Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia, Zanzibar ambayo yatawasaidia wanafunzi wa chuo hicho kwenye masomo yao kama mbadala wa nishati  katika kipindi ambacho Umeme umekatika.

 Mkuu wa Zantel, Zanzibar Mohamed Mussa Baucha, akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi majenerata matatu kwa Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia, mwishoni mwa juma mjini, Zanzibar. Majenereta hayo yana lengo la kuwasaidia wanafunzi wa chuo hicho kwenye masomo yao kama mbadala wa nishati  katika kipindi ambacho Umeme umekatika. Pamoja nae tokea kushoto ni Afisa Mkuu wa Biashara Zantel, George Lliakopoulos, Afisa Mkuu wa Masuala ya Fedha Zantel, Jean-Paul Happart na Kulia ni Afisa Mkuu wa Masuala ya Ufundi na Teknolojia Zantel, Larry Arthur.
 Mwanafunzi wa Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia, Zanzibar Abdukadir Mkubwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar mwishoni mwa juma wakati wa hafla ya kupokea majenerata matatu kutoka Zantel yatakayowasaidia wanafunzi wa chuo hicho katika masomo yao kama mbadala wa nishati hasa kipindi ambacho Umeme umekatika.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia, Zanzibar Abdulhamid Idrissa Haji (katikati) akimpongeza Afisa Mkuu wa Masuala ya Ufundi na Teknolojia Zantel, Larry Arthur hivi karibuni mjini Zanzibar na kumshukuru kwa msaada mkubwa ambao Chuo hicho wameupata kutoka Zantel. Zantel walikabidhi msaada wa majenerata matatu yatakayowasaidia wanafunzi wa chuo hicho katika masomo yao kama mbadala wa nishati hasa kipindi ambacho Umeme umekatika


ZANTEL imetoa msaada wa majenereta tatu zilizotumika kwa Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia, Zanzibar mwishoni mwa juma mjini Unguja.

Majenereta hayo yenye ambayo yamekwishatumika yenye thamani ya dola 250,000 yamekabidhiwa kwa Taasisi hiyo ili kusaidia jitihada za Chuo hicho katika kuhakikisha wanafunzi wanaendelea na masomo yao kipindi ambacho Umeme umekatika.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano mwishoni mwa juma mjini Unguja, Mkuu wa Kampuni ya Zantel, Zanzibar, Ndugu Mohamed Mussa Baucha alisema mchango huo una lengo la kuwasaidia wanafunzi wa chuo na masomo yao kama mbadala wa nishati hasa kipindi Umeme unapokua umekatika huku akitumai kwamba wanafunzi wa chuo hicho, watahimizwa kufanya vizuri kutokana na msaada huo.

"Ni jambo la furaha na faraja kwetu kutoa msaada wa majenereta kwa Taasisi hii, na tumaini letu kubwa ni kuwa yatakuwa msaada muhimu kwa wanafunzi katika masomo yao," alisema Baucha.

Aliongeza kuwa ZANTEL imekuwa msatari wa mbela katika kujitolea na itaendelea kuwekeza katika miradi mbalimbali endelevu na kuunga mkono mipango inayozingatia kuboresha elimu nchini.

Abdulhamid Idrissa Haji, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo alisema kuwa msaada huo umekuja kwa wakati muafaka kwa sababu chuo chake hakikuwa na vyanzo mbadala vya nishati, mara umeme unapokuwa umekatika, kitu ambacho kiliwasababishia wanafuzi wengi usumbufu.

"Ukosefu wa umeme vyuoni, hukatisha morali ya wanafunzi hasa hasa kwa masomo ya sayansi na uwezo wa kuyaelewa masomo hayo kwa usahihi."

Aliishukuru Zantel kwa msaada wao muhimu katika kuboresha ubora wa elimu nchini na kuhimiza makampuni mengine kufuata mfano huo.

“Msaada huu sio chachu tu katika ufaulu wetu kitaaluma bali pia utaongeza morali kwa wanafunzi,” alihitimisha Haji.

Mwanafunzi wa chuo hicho aliyefahamika kwa jina Abdulkadir Mkubwa Khamis ambaye anachukua masomo ya sayansi, alisema mchango wa Zantel utawawezesha kuboresha utendaji wao na pia kutatua baadhi ya changamoto ambazo zilikuwa zinawakabili hapo awali.

"Matatizo ya umeme huathiri sana masomo yetu, lakini kwa msaada huu, natumai matatizo hayo yatapungua," alihitimisha.

Mwaka jana, Kampuni ya Zantel ilitoa vitabu vyenye thamani ya 10M/- kwa Taasisi hiyo katika jitihada za kupunguza uhaba wa vifaa vya kufundisha na kujifunzia chuoni hapo.

KWA MAELEZO ZAIDI:

Rukia Mtingwa

Baruapepe: r.mtingwa@zantel.co.tz

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.