Habari za Punde

MASAUNI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI KUJADILI UPUNGUZAJI WA AJALI

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Waziri Wizara ya  Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa  kikao cha kujadili mikakati ya kupunguza tatizo la ajali za barabarani.Kikao hicho kimefanyika  katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam
 Katibu wa Baraza la Taifa la Usalama  Barabarani,  Mkuu  wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Fortunatus Musilimu (kulia meza kuu), akizungumza wakati wa  kikao cha kujadili mikakati ya kupunguza tatizo la ajali za barabarani.Kikao hicho kimefanyika  katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam
 Mjumbe kutoka Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Geoffrey Silanda,   akichangia hoja wakati wa wakati wa  kikao cha kujadili mikakati ya kupunguza tatizo la ajali za barabarani.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.Wengine ni Mwakilishi kutoka Wizara ya Elimu, Hidaya Mohamed na Mwakilishi kutoka Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania(TABOA), Elimboto Mtatulu (kushoto).
Wajumbe wa kikao kinachojadili mikakati ya kupunguza tatizo la ajali za barabarani kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Waziri Wizara  ya  Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), wakishiriki  kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.