Habari za Punde

SIKU SABA ALIZOTOA WAZIRI KIGWANGALLA ZAZAA MATUNDA


Wiki chache zilizopita Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Hamisi Kigwangalla alitoa siku saba kwa polisi kukamata watuhumiwa wa mauaji ya mwanaharakati dhidi ya mauaji tembo Wayne Lotter, pia alitaka nyumba zilizouzwa kinyemela huko Arusha zirudishwe na pia alitoa siku saba kwa wakurugenzi wa kampuni nne za uwindaji kukutana nae Dodoma.
Jana kwenye kipindi cha 360 Waziri Dk. Kigwangalla alitoa maelezo ya kina kuhusu maelekezo aliyotoa na pia kuelezea mikakati mbalimbali ya Wizara yake. Kuhusu mauaji ya Lotter alisema kuwa watuhumiwa walikamatwa na kufikishwa mahakamani. Alimsifu IGP Sirro kwa ushirikiano na Wizara yake.
Alieleza kuwa Katiba inatambua Waziri kama sehemu ya Serikali na kwamba Polisi wapo ili kusaidia Serikali kutimiza malengo yake. Kuhusu nyumba za Arusha, alieleza kuwa ushahidi unaonyesha wazi kuwa waliotajwa walikuwa wamiliki wao binafsi au kupitia familia zao. Waziri Dk.Kigwangalla alieleza mkakati wa kufungua na kukuza utalii kusini mwa Tanzania.
Alieleza mradi wa regrow ambao utawezesha sekta ya kukua kusini mwa Tanzania. Pia alizung umzia umuhimu wa uhifadhi na kueleza kuwa mto Ruaha kwa sasa unakauka kwa siku 60 wakati wa kiangazi na malengo ni kurejesha hadi kukauka kwa siku 10 tu. Kuhusu kutangaza vivutio, Waziri Dk.Kigwangalla alieleza mkakati wa kutangaza vivutio na pia uanzishwaji wa mwezi wa urithi ambao sio tu utaongeza vivutio vya utalii bali utaenzi tamaduni na mila za Kitanzania

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.