Habari za Punde

Waziri Mkuu Majaliwa alipokutana na Rais wa FIFA Giovanni Infantino

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Kassim Majaliwa (katikati) akimskiliza Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Giovanni Vincenzo ‘Gianni’ Infantino alipomkaribisha ofisini kwake, Magogoni, Dar es Salaam jana. Kulia ni Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad
Waziri Mkuu, Dk. Kassim Majaliwa akimsikiliza Rais wa CAF, Ahmad. Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe na kushoto Rais wa FIFA, Gianni Infantino  
Dk. Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya kiwango Rais wa CAF, Ahmad raia wa Madagascar  
Hapa Gianni Infantino akiteta jambo na Ahmad ukumbi wa mikutano, Ofisi ya Waziri Mkuu 
Mtaliano Gianni Infantino (kulia) na Ahmad wakisoma hotuba ya Dk Kassim Majaliwa iliyotafsiriwa Kiingereza kutoka Kiswahili  
Waziri Mkuu, Dk Kassim Majaliwa akihutubia kwa Kiswahili jana 
Gianni Infantino alimkabidhi jezi Waziri Mkuu, Dk. Kassim Majaliwa  
Jezi namba tisa (9) tena yenye jina, Majaliwa ndiyo Rais huyo wa FIFA alimkabidhi Waziri Mkuu wa Tanzania 
Gianni Infantino akimkabidhi zawadi nyingine Waziri Mkuu, Majaliwa jana 
Waziri wa Habari 'Mtanashati' Dk Harrison Mwakyembe akiwaongoza kuondioka ukumbini Gianni Infantino na Ahmad baada ya mkutano na Waziri Mkuu. Wawili hao walikuwa nchini tangu juzi hadi jana kwa ajili ya Semina ya FIFA iliyofanyika Dar es Salaam ikishirikisha nchi 21 duniani, wakiwemo wenyeji, Tanzania  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.