Habari za Punde

Dalali Ataka Tawi la Simba Cream Tanga Kuazisha Timu ya Vijana U-17 ALIYEKUWA Mwenyekiti  wa Simba, Hassani Dalali akizungumza na wapenzi,wanachama na wakereketwa wa  tawi la Simba Cream la Jijini Tanga wakati alipolitembelea ikiwemo kuhimiza umoja na mshikamano ili kuiwezesha timu hiyo kuchukua ubingwa msimu huu
 ALIYEKUWA Mwenyekiti  wa Simba, Hassani Dalali akizungumza na wapenzi,wanachama na wakereketwa wa  tawi la Simba Cream la Jijini Tanga wakati alipolitembelea ikiwemo kuhimiza umoja na mshikamano ili kuiwezesha timu hiyo kuchukua ubingwa msimu huu kushoto ni Mwenyekiti wa Tawi hilo John Bukuku kulia ni Katibu akifuatiwa na katibu Msaidizi na Mwekahazina wa Tawi hilo Edgar Mdime
 Katibu Msaidizi na Mwekahazina wa Tawi la Simba Cream la Jijini Tanga Edgar Mdime akisoma risala fupi katika ziara ya Aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba Hassani Dalali iliyokuwa na lengo la kuhimiza umoja na mshikamano ili kuiwezesha timu hiyo kuchukua ubingwa msimu huu
 Katibu Mkuu wa Tawi hilo akizungumza machache
 Sehemu ya wapenzi,wakereketwa na wanachama wa klabu ya Simba wakimsikiliza Dalali
 Mmoja wa wanachama wa Simba kutoka Tawi la Simba Cream Chongowe akiuliza swali
  Katibu Msaidizi na Mwekahazina wa Tawi la Simba Cream la Jijini Tanga Edgar Mdime akiteta jambo na mwanachama wa tawi hilo
 Sehemu ya wapenzi,wakereketwa na wanachama wa klabu ya Simba wakimsikiliza Dalali
Sehemu ya wapenzi,wakereketwa na wanachama wa klabu ya Simba wakimsikiliza Dalali
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba Hassani Dalali katika akiwa kwenye picha ya pamoja na wapenzi,wanachama na wakereketwa wa Simba Jijini Tanga
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba Hassani Dalali akiwa kwenye picha na Katibu Msaidizi wa Tawi la Simba Cream la Jijini Tanga Edgar Mdime ambaye pia ni Mweka Hazina wa Tawi hilo
ALIYEKUWA Mwenyekiti  wa Simba, Hassani Dalali amelitaka tawi la Simba Cream la Jijini Tanga kuanzisha timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ili iweze kuwa hazina kubwa ya wachezaji kwa siku za mbeleni.
Licha ya hivyo lakini pia inasaidia kuweza kuinua vipaji vya wachezaji wachanga ambao wanaweza kuonekana thamani yao siku zinazokuja kwani mkoa wa Tanga una vipaji vya soka vingi.
Dalali aliyesema hayo juzi akizungumza na wanachama wa Simba ikiwemo kuhimiza umoja na mshikamano ili kuiwezesha timu hiyo kuchukua ubingwa msimu huukatika tawi la Simba Cream la Tanga mjini ambalo lilianzishwa mwaka 2013 na kuzinduliwa na aliyekuwa Rais wa Simba Evans Aveva.

Alisema uanzishwaji wa timu hiyo utakuwa na faida kubwa kwa kusaidia timu hiyo kuwa na hazina ya wachezaji ambao wanaweza kuwatumia kwa miaka ijayo ili kuendelea kuwika kama ilivyokuwa miaka ya nyuma hapa nchini.

“Kwani timu hiyo inapoanzishwa na kuweza kuwa imara itatuwezesha tunapotaka wachezaji tunakuja kuchukua mkoani Tanga kwa sababu tutakuwa tumewekeza mtaji mkubwa wa vijana”Alisema.

Hata hivyo alisema tawi la Simba la Kinondoni kwa miaka ya nyuma ndio ambalo liliwasaidia kuwapelekea mchezaji Uhuru Selemani na baadae yeye kumpeleka kwenye klabu ya Coastal Unon .
(Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.