Habari za Punde

TSN na Baraza la Biashara Zanzibar Laandaa Kongamano la Fursa Kwa Wajasiriamali Zanzibar. Tarehe, 16/17/3/2018.

Meneja Mauzo na Masoko wa TSN Januarius Sebastian Maganga akizungumza na Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali vya Zanzibar kukamilika kwa Kongamano la Kuwawezesha na kutowa Fursa kwa Wajasiriamali wa Zanzibar linalotarajiwa kufanyika kwa Siku mbili katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Zanzibar na kuwashirikisha wadau mbalimbali wanatoa mada kwa Wajasiriamali wa Zanzibar ili kuweza kupata fursa za kukuza biashara zao. Kongamano hilo limeandaliwa kwa ushirikiana na Baraza la Biashara Zanzibar na TSN. 


Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo wa maandalizi ya Kongamano la Fursa za Biashara kwa Wajasiriamali wa Zanzibar. mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari kikwajuni Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.