Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni, akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kilwa Kusini(hawapo
pichani), wakati wa mkutano wa hadhara ambapo aliwaasa wananchi hao
kushirikiana na vyombo vya Ulinzi na Usalama kufichua wahalifu ikiwa ni
kuisaidia serikali katika adhma ya kukomesha matendo ya uhalifu nchini.Mkutano
huo umefanyika katika Viwanja vya Maalim Seif,Kilwa Kusini
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi,
Christopher Ngubiagai akizungumza na
wananchi wa Wilaya ya Kilwa Kusini(hawapo pichani), wakati wa ziara ya Naibu
Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni.Mkutano huo umefanyika
katika Viwanja vya Maalim Seif,Kilwa Kusini.
Mwananchi wa Kilwa Kusini, Said Saleh,
akimuuliza swali Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad
Masauni(hayupo pichani), kuhusu kukamatwa na polisi kwa ndugu zao wanaotuhumiwa kwa uhalifu.Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mwananchi wa Kilwa Kusini, Rehema Said ,
akimuuliza swali Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad
Masauni(hayupo pichani), kuhusu uhalifu wanaofanyiwa wanawake ikiwemo kubakwa
na kuporwa pesa na mali na wahalifu
Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na baadhi ya wananchi wa
Wilaya ya Kilwa Kusini baada ya kumaliza mkutano wa hadhara ambapo aliwaasa
wananchi hao kushirikiana na vyombo vya Ulinzi na Usalama kufichua wahalifu
ikiwa ni kuisaidia serikali katika adhma ya kukomesha matendo ya uhalifu
nchini.
Wananchi wa Wilaya ya
Kilwa wakimsikilza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni(hayupo pichani), akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara ambapo
aliwaasa wananchi hao kushirikiana na vyombo vya Ulinzi na Usalama kufichua
wahalifu ikiwa ni kuisaidia serikali katika adhma ya kukomesha matendo ya
uhalifu nchini.Mkutano huo umefanyika katika Viwanja vya Maalim Seif,Kilwa
Kusini.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
IMEANDALIWA
NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI -WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment