Habari za Punde

Uzinduzi wa Kongamano la Fursa za Biashara kwa Wajasiriamali Zanzibar. :Balozi Seif Fursa za Uchumi Zanzibar Hazijatangazwa Ipasavyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Biashara kwa Fursa ya Wajasiriamali Zanzibar, akimuwakilisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Zanzibar na kuwashirikisha Wajasiriamali 350. katika kongamano hilo lililoandaliwa na Shirika la Magazeti ya Serikali Tanzania TSN. Na kushirikiana na Tamasha la Biashara Zanzibar.
Waziri wa Biasha na Viwanda Zanzibar Mhe. Balozi Amina Salum Ali akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi kikwajuni Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud akizungumza wakati wa uzinduzi wa hafla hiyo ya Kongamano la Biashara la Fursa kwa Wajasiriamali wa Zanzibar.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Tanzania Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa uzinduzi wa hafla ya Kongamano la Tano la Fursa kwa Wafanyabiashara na Wajasiriamali wa Zanzibar kupata fursa za kibiashara lililoandaliwa kwa pamoja na TSN na Tamasha la Biashara Zanzibar.
Mhariri Mtendaji wa Shirika la Magazeti ya Serikali Tanzania TSN Dkt.Jim Yonazi akizungumza na kutowa maelezo ya mafanikio ya Makongamano ya Fursa za Wafanyabiashara na Wajasiriamali wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Tano linalofanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi kikwajuni Zanzibar.
Mabalozi wadogo wanaowakilisha Nchi zao Zanzibar wakifuatilia ufunguzi wa Kongamano hilo la Biashara kutowa fursa za Kibiashara Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.