Habari za Punde

MIGOMBA MABINGWA KOMBE LA SIRRO CUP 2018 KIBITI

Msanii Malima Ndolela akitumbuiza wakati wa sherehe za kufunga Michezo ya kuwania kombe la IGP Sirro (Sirro Cup 2018 Kibiti) katika uwanja wa Samora Kibiti. Timu ya Migomba kutoka Rufiji ililifanikiwa kutwaa ubingwa baada ya kuichapa Mjawa penati 12 kwa 11.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarest Ndikilo akisalimiana na Wachezaji wa timu ya Migomba kutoka Rufiji kabla ya kuanza kwa fainali ya kombe la IGP Sirro (Sirro Cup 2018 Kibiti) iliyoikutanisha timu hiyo na Mjawa kutoka Kibiti katika uwanja wa Samora Kibiti. Migomba walifanikiwa kutwaa ubingwa baada ya kuichapa Mjawa penati 12 kwa 11.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarest Ndikilo akisalimiana na Wachezaji wa timu ya Mjawa kutoka Kibiti kabla ya kuanza kwa fainali ya kombe la IGP Sirro (Sirro Cup 2018 Kibiti) iliyoikutanisha timu hiyo na Migomba kutoka Rufiji katika uwanja wa Samora Kibiti. Migomba walifanikiwa kutwaa ubingwa baada ya kuichapa Mjawa penati 12 kwa 11.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Chatanda akimkabidhi seti jezi nahodha wa timu ya Mjawa Bakari Tuga kutoka Kibiti baada ya kushika nafasi ya pili katika kombe la IGP Sirro (Sirro Cup 2018 Kibiti) iliyoikutanisha timu hiyo na Migomba kutoka Rufiji katika uwanja wa Samora Kibiti. Migomba walifanikiwa kutwaa ubingwa baada ya kuichapa Mjawa penati 12 kwa 11

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarest Ndikilo akimkabidhi kombe la ushindi nahodha wa timu ya Migomba Maulid Mtupa baada ya kuibuka mabingwa wa kombe la IGP Sirro (Sirro Cup 2018 Kibiti) kwa kuichapa Mjawa  kwa penati 12 kwa 11 katika uwanja wa Samora Kibiti. (Picha na Jeshi la Polisi).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.